MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (NGOs Tanzania Bara) na Balozi wa Covid19 Tanzania, Mhe Neema Lugangira akizungumza wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa COVID19 tarehe 12 Agosti 2021

MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (NGOs Tanzania Bara) na Balozi wa Covid19 Tanzania, Mhe Neema Lugangira akizungumza wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa COVID19 tarehe 12 Agosti 2021

MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (NGOs Tanzania Bara) na Balozi wa Covid19 Tanzania, Mhe Neema Lugangira amesema Wabunge wana nafasi ya kipekee ya kuweza kuihamasisha jamii kwa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kujikinga na Ugonjwa wa COVID19 kupata Chanjo.

Mbunge Lugangira aliyasema hayo wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa COVID19 tarehe 12 Agosti 2021 ambapo alisema Wabunge wakipatiwa elimu itakuwa ni rahisi kwao kuifikisha kwa jamii ikiwemo kuondosha dhana potofu iliyopo miongoni mwa jamii kuhusu chanjo hizo.

Alisema upo umuhimu wa Wabunge kupatiwa elimu kwa sababu wana jukumu la kuwa sehemu ya mafanikio  ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID19

“Naomba nisema wazi kuwa ndio Chanjo ya COVID19 ni hiari lakini kwa nafasi zetu kama Wabunge hatupaswi kutumia hiari yetu kama kigezo cha kuwafanya wananchi wasitumie hiari yao na tunatakiwa tuwaelemishe kwa usahihi ili kila mtu atumie hiari yake ya kupata Chanjo ya COVID19” Alisema kwa hisia kali.

Hata hivyo aliwapongeza sana Wabunge wenzake kwa kuwa mstari wa mbele kuchoma Chanjo ya COVID19 wao wenyewe na kuhamasisha wananchi wa majimbo na mikoa yao kuchoma Chanjo ya COVID19.

Alisema kwa niaba yao anaomba moja ya Maazimio ya Mdahalo huo iwe ni kuja na utaratibu wakuwaelimisha na kuwatumia Wabunge katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa COVID19 kama inavyofanyika kwa makundi mengine.

Hata hivyo alisema akiwa kama Mbunge kijana anatoa pongezi nyingi kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea Chanjo na yeye mwenyewe kukubali Chanjo ya COVID19, kuchanjwa mubashara huku wananchi na dunia ikushuhudia  kitendo kilichodhihirisha pasi na shaka kuwa Chanjo ya COVID19 ni salama.

Alisema kwamba tokea Wimbi la Kwanza la COVID19 hadi sasa Wimbi la Tatu, Kirusi cha COVID19 kimeshajibadilisha sana na kila kinapojibadilisha kinazidi kuwa hatari.

Aliongeza kwamba hali hii ilipelekea dunia kuona njia  pekee ya kukabiliana na Kirusi kinachosababisha Ugonjwa wa COVID19 na kupunguza makali yake hata pale utakapoipata ni Chanjo ya COVID19.

Hivyo, kwakuwa Tanzania sio Kisiwa ilikuwa ni muhimu pia wafanye tathmini juu ya Ugonjwa wa COVID19 na nini kifanyike kama Taifa na kwa mara nyingine tena na Mbunge Neema Lugangira alimpongeza sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa Maamuzi Sahihi na Wakati Sahihi wakuleta Chanjo ya COVID19 nchini.

Mara baada ya kuhitimisha Hotuba yake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alisimama na kukiri kutambua kazi kubwa ambayo Mbunge Neema Lugangira amefanya katika kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu kujikinga na Ugonjwa wa COVID19 tokea Wimbi la Kwanza na hadi katika Wimbi la Tatu na kuendelea kuemilisha na kuhamasisha jamii kuhusu Chanjo ya COVID19 hivyo alimteua kuwa Balozi wa COVID19 Tanzania.

- MWISHO -
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: