Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda (wa pili kutoka kushoto) Akizungumza na Washindi wa mashindano hayo na wanafunzi wengine walioshiriki kwenye hafla hiyo, Kushoto ni Meneja wa CRDB tawi la SUA Isabela Kitila.

Mshindi wa kwanza kwenye mashindano hayo ambaye amepatiwa laptop Megan Manase Mushi akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washindi wenzake.

Meneja wa Benki ya CRDB tawila la SUA Isabela Kitila akieleza namna washindi hao walivyopatikana kabla ya zoezi la utoaji wa zawadi.

Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda (Katikati) akimkabidhi mshindi wa Simu Abeid Naftari Mtemi simu yake na kushoto ni Meneja wa CRDB tawi la SUA.

Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda (Katikati) akimkabidhi Mshindi wa laptop Megan Manase Mushi laptop yake na kushoto ni Meneja wa CRDB tawi la SUA.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala (mwenye tai nyekundu) akiwa Mshauri wa wanafunzi SUA Bwana Pure Mulshabi na viongozi wengine wa SUA na CRDB wakati wa afya hiyo.

Washindi wa shindano hilo wakiwa kwenye picha ya Pamoja na mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda pamoja na Viongozi wa CRDB na Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi SUA yaani SUASO.

Wanafunzi na viongozi wa wanafunzi SUASO wakifuatilia tukio hilo la utoaji wa zawadi kwa wenzao.


Na: Calvin Gwabara – Morogoro.

Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amewataka Wanafunzi wa Chuo hicho kufungua akauti katika Taasisi za Kifedha ili kuweza kuwajengea nidhamu ya fedha wanazo zipata kutoka bodi ya mikopo na kwa Wazazi.

Ushauri huo ameutoa wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi watatu ambao wameshinda zawadi za Tanakilishi mpakato yaani (LAPTOP mbili na Simu janja moja zilizotolewa na Benki ya CRDB tawi la SUA kutokana na kufanya miamala mingi kupitia akauti zao za SCHOLAR ACCOUT.

“Mimi niwapongeza kwa kuweza kushinda, nyinyi ni vijana lakini mkae mkijua ujana unapita na majukumu yanazidi kuongezeka ni vizuri kujiwekea utamaduni wa kutumia taasisi za kifedha wale ambao mmeamua kwenda CRDB kungua hizi akauti nawapongeza sana matumiani yangu ni kwamba hitawajengea nidhamu ya matumizi mazuri ya fedha mnazo zipata”Alisema Prof .Chibunda.

Prof. Chibunda fedha amesema ambazo wanazipata kutoka kwenye bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, amewakumbusha kuwa ni kweli zile ni za mkopo na mkopo siku zote unapaswa utumike kwa tahadhali na kwa malengo ambayo yamekusudiwa hivyo wawe makini kwenye matumizi na kukumbuka kuzirudisha wamalizapo chuo ili zisaidia Watanzania wengine.

Ametumia pia nafasi hiyo kuwakumbusha Wanafunzi wote kuchukua tahadhari katika wakati huu ambao jamii serikali na wataalamu wa afya wanakumbusha kuchukua tahadhari zote za maambukizi ya Ugonjwa wa COVID 19 kama ambavyo inashauriwa na wasifanye mzaha maana Chuoni kuna wanafunzi wengi.

“Sisi kama Chuo tumeweka maji ya kunawa kila kona ya Chuo chetu ili Wanafunzi waweze kupata huduma za kunawa mikono na tunaomba msipuuze naweni mikono na msione aibu kuvaa barakoa vaeni kama mnazo ili mjikinge nyinyi na na kuwakinga wenzenu pia|” Alisisitiza Prof. Chibunda.

Kwaupande wake Meneja wa Benki ya CRDB tawila la SUA Isabela Kitila amesema CRDB imweza kubuni na kuja na akauti hiyo ya SCHOLAR ACCOUT ili kuweza kumsaidia Mwanafunzi kipindi anapokuwa Chuoni katika kipindi chake cha masomo.

“Hii akauti haina makato ya mwezi kwahiyo mwanafunzi anapofanya miamala yake anakuwa huru kwasababu tunajua Mwanafunzi anakuwa na mambo mengi vilevile tunafahamu uchumi wa Mwanafunzi ndio maana tumeweza kuja na hii ili kuweza kupunguza chaji za mwezi za makato, Akauti hii pia Mwanafunzi anaweza kuitumia mahali popote ata akiwa tayali ameajiriwa” Alifafanua Isabela.

Akizungumzia manufaa yatokanayo na akaunti hiyo ya SCHOLAR Isabela amesema kuwa inaweza kumsaidia Mwanafunzi kupata mkopo wa awali kupitia Benki ya CRDB ili aweze kutatua changamoto zinazomkabili na kuweza kulipa pale atakapo pata mkopo kutoka Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu.

“Vilevili utaweza kupata huduma mbalimbali kupitia benki yetu ya CRDB kama Simu benking,internet benking, na kuweza kufanya manunuzi ya mtadaoni ukiwa Chuoni na unamkopo ni vizuri kujiifadhia fedha kidogo unapo maliza Chuo anagalau na wewe unakuwa na fedha ambazo utaweza kuanzia maisha mtaani ”.Aliongeza Meneja huyo wa CRDB Tawi la SUA.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi ambao wameshinda zawadi hizo Megan Manase Mushi wamesema kupata Tanakilishi (Laptop) zitawasaidia katika kufanyia shughuli mbalimbali za kimasomo maana hawakuwa nazo kabisa hivyo CRDB imekuwa mkombozi katika kuwapatia vitendea kazi hivyo.

Paia wamewataka Wanafunzi wengine kujiunga na Benki ya CRDB kwani kwani imekuwa ina huduma nyingi nzuri kwaajili ya wanafunzi ambazo zitawasaidia katika kutunza fedha na kuzitumia vizuri pindi wanapozihitaji maana kila mahali sasa wanapatikana.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: