Na,Raheem Mohamed Tunduma


IKIWA ni wiki mbili Sasa toka shule za Msingi na Sekondar nchini kufunguliwa, shule ya mchepuo wa Kiingereza iliyoanzishwa na Halmashauri ya mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe yafanikiwa kuanza kwa mafanikio makubwa ya wanafunzi kutokana na wazazi wengi kuitikia wito na kupeleka watoto wengi kuanza  darasa la kwanza na awali kwa mwaka wa masomo wa 2021.


Akizungumza na mwandishi  aliyetembelea shule hiyo mpya ya mchepuo wa kiingereza afisa elimu idara ya elimu Msingi mji wa Tunduma Mtafya Wilson alisema licha ya shule hiyo kufunguliwa  januar ,11 mwaka huu kuwa mwitikio wa wazazi umekuwa mkubwa na kufanikiwa kuvuka lengo ambalo walijiwekea.

Alisema kwa mwaka huu wa 2021 baada ya kuifungua shule hiyo walipanga kuanza na wanafunzi wa darasa la Kwanza 45 sawa na mkondo mmoja na wanafunzi wa awali 90, lakini mpaka Sasa wanafunzi walioanza masomo kwa darasa la Kwanza ni 64 na awali ni 35 huku waliendelea kuongezeka kila siku.


"Mwitikio ni mkubwa Sana ndani ya wiki mbili tumepata idadi kubwa ya wanafunzi ambapo darasa la Kwanza tumevuka lengo hivyo tunategemea kuwa na mikondo miwili tofauti na ambavyo tulikuwa tumekadiria kuwa na mkondo mmoja,

Mpaka Sasa tuna wanafunzi zaidi ya 90 , hivyo kufikia mwezi wa tatu mwaka huu ambapo kitaratibu ndio mwezi wa ukomo wa kupokea na kuwasajili wanafunzi tutakuwa na idadi kubwa zaidi ya wanafunzi kutokana na mwitikio uliojitokeza hivi mwanzoni" alisema Afisa elimu.


Kuhusu miundo mbinu shuleni hapo alisema tayar wana mdarasa manne ambayo tayari yamekamilika, bwalo la chakula ambalo linatumika kwa chakula Cha mchana na uji asubuhi, wanawachemshia maji ya kunywa ambayo yanachotwa na kuletwa na gari wakati wakijiandaa kuchimba visima vya muda mrefu.


Mtafya aliongeza kuwa tayari wamepata gari kwa ajili ya kuwasafirisha wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali katika halmashaur za mkoa wa Songwe, wakati huo huo wakijipanga kujenga kukamilisha mabweni kwa wanafunzi ambao watakaa bweni kwa mwaka ujao wa masomo.


 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Dany Mbembela alisema  Shule hiyo inawalimu watano ambao wanatosha kabisa kwa uwiano wa wanafunzi ambao wapo shuleni na ambao wanazidi kuongezeka ili kuhakikisha taaluma ina kuwa vizuri kuzidi hata shule za watu binafsi.


"Tunauhakika shule hii itafanya vizuri kushinda shule za binafsi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri muda mrefu, tumejipanga kushindana na shule zote ambazo hufanya vizuri katika ufaulu darasa la nne na darasa la Saba" alisema Mbembela.


Kwa upande wake Mdhibiti Ubora elimu katika wilaya Momba Kenani Mwalongo alisema shule hiyo imejengwa vizuri na imekidhi vigezo vyote kwa kuwa na miundombinu mizuri ikiwa ni oamoja na vifaa na zanaa za kufundisha kwa watoto wadogo wa dara la awali na darasa la Kwanza.


Aidha alisema katika wilaya ya Momba yenye halmashaur mbili za Momba na Tunduma , kwa upande wa Halmashaur ya Wilaya ya Momba kuna changamoto kubwa ya watoto wengi kutomaliza shule kutokana na uelewa mdogo wa wazazi wao kuhusu umuhimu wa shule, Jambo ambalo hupelekea matokeo ya darasa la Saba kutokuwa mazuri ukilinganisha na Halmashauri ya Tunduma.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashaur ya mji Tunduma Regina Bieda alisema lengo kubwa la kuanzisha shule hiyo ya mchepuo wa kiingereza ni kuwasaidia Wananchi mji wa Tunduma na Mkoa wa Songwe kuhakikisha wanapata nafasi ya kuwasomesha watoto wao katika shule nzuri kutokana na uhitaji wa shule za aina hiyo kuwa mkubwa .


Bieda alisema lengo lingine kuwa ni kuiongezea halmashaur hiyo ya mji mapato kupitia ada za wanafunzi ,ambapo mapato hayo yatasaidia kuimalika kwa huduma mbalimbali kama vile ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, hospital pamoja na huduma za maji.


Mwisho

Share To:

msumbanews

Post A Comment: