NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Kamshna mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Dkt Edwin Mhede amesema kuwa mamlaka hiyo haiongezi muda wa wafanyabiasha kuboresha mashine za EFD badala yake itachukua hatua za kisheria kwa ambao bado hawajaboresha.


Dkt Mhede aliyasema wakati akifungua mkutano mkutano mkuu wa nusu mwaka wa mamlaka hiyo ambapo  alipokea dodoso la kuomba kuongezwa muda wa wafanyabiasha kuboresha mashine za EFD na kusema kuwa  jambo hilo haliwezekani  kwani zoezi hilo linaweza kufanyika kwa muda mfupi na walipewa muda wa kutosha kuanzia Desemba 7, 2020 hadi Januari 7,2021.


Alieleza kuwa ombi hilo amelikataa na wafanyabiashara wote ambao bado wachukuliwe hatua kwani wakianza kutengeneza mazingira ya kuongeza muda watakuwa wanacheza na hawatafikia lengo la uboreshaji huo.


“Suala la EFD mashine zenye protocol  2.1 sio chagua  lazima,  haya maboresho ni lazima yaendane na aina ya mashine tunazozitumia hivi sasa na  upatikanaji wake ni wa dakika chache kwahiyo nasema kuongeza muda ni jambo ambalo haliwezekani inajulikana wazi kuwa utiifu wakati mwingine lazima watu walazimishwe,” Alisema Dkt Mhede.



Alifafanua kuwa kama upatikanaji EFD  hauzidi wa masaa mawili au matatu na waliwapa mwezi mzima ni kwanini waongeze muda, ambapo aliagiza baada ya kutoka katika mkutano huo wakachukue hatua kwani hawatakuwa na namna nyingine zaidi ya kwenda kuwapa motisha watii kwa mujibu wa sheria lakini suala la  kuongeza muda hicho kitu hakitakuwepo.


Alieleza kuwa ni lazima wahakikishe kwamba walipa kodi na wanaofanya manunuzi wanatii kifungu cha sheria cha 36 cha sheria ya usimamizi wa kodi kwa kutoa risiti sahihi za EFD ambapo uboreshaji huo utasaidia ukusaji sahihi wa mapato hivyo kama nia ilikuwepo kwanini itumike muda mwingi.



Kwa upande wake Meneja wa EFD wa mamlaka hiyo Mabula Sambayukha alisema kuwa watumiaji wote wa EFD wahakikishe wanaboresha mashine zao ili kuendana na mfumo mpya wa TRA ambapo manufaa ya uboreshaji huo ni pamoja na kusaidia hata wanunuazi kuwa na uhakika na uhalali wa risiti wanazopata kwa kuscan QR code.


Naye naibu  kamishina wa mamlaka ya mapato Tanzania ,(TRA) Msafiri Mbibo alisema kuwa mkutano huu utasaidia kuweza  kujua namna ya kutatua matatizo  yaliopo katika sekta yao ,pamoja na kupanua mikakati itakayo saidia kupata mapato mengi  yatakayo wezesha kufikia malengo waliojiwekea.


Alibainisha kuwa kazi ya taasisi  hii ni kuweza kusaidia serikali kujenga taifa linalojiweza kiuchumi pamoja na kimaendeleo.


Aliongeza kuwa mkutano huo utasaidia kuwawezesha kujadili njia bora itakayosababisha utendaji kazi kuwa mzuri ,ambapo pia watajadili namna ya kutatua matatizo waliyonayo ikiwemo upungufu wa idadi ya Wataalam wa mamlaka hiyo , upungufu wa vitendea kazi pamoja pamoja na ukosefu wa nyumba za wataalam wanaoishi maeneo ya mipakani.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: