Ferdinand Shayo ,Manyara


Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Joseph Mkirikiti ametembelea kiwanda cha Mati Super Brands Limited Mkoani Manyara na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa mbali mbali ikiwemo vinywaji vikali pamoja kufanya mazungumzo yanayolenga kuboresha mazingira ya wawekezaji wa viwanda mkoani hapa.


Mkirikiti amepongeza juhudi za wawekezaji hao ambao wameweza kuajiri vijana zaidi ya 100 pamoja kulipa kodi kwa serikali ambayo inasaidia kuchochea maendeleo ya mkoa huo na taifa kwa ujumla.


Aidha ameahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji hao kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya biashara pamoja na kuboresha miundombinu.


Mhasibu Mkuu wa Kiwanda cha Mati Super Brands Limited Goodluck Silayo  amesema kuwa kiwanda hicho kitazindua bidhaa mpya inayokwenda kwa jina la Tanzanite ikiwa ni kupanuka kwa wigo wa uzalishaji na mapinduzi ya ubora wa bidhaa.


Silayo amesema kuwa mwezi wa pili mwaka huu wana mpango wa kuongeza ajira mpya kwa vijana baada ya kupanua uzalishaji katika viwanda vipya vilivyopo chini ya kampuni hiyo.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Wafanyakazi wa Kiwanda hicho James Mollel amesema kuwa kiwanda hicho kimewapa fursa ya ajira kwani awali vijana wengi walikua wamehimu na hawakua na kazi hivyo wameweza kujipatia kipato na kujiletea maendeleo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: