Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi mwenye miwani akiongea na akina mama wafanya biashara ya viazi lishe   wa Kitongoji cha Kideka kijiji cha Nkunikana kuhusu kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona-Covid 19 kulia Mkuu wa Wilaya ya Ikungi  Edward Mpogolo kushoto Mkurugenzi Mtendaji Justice Kijazi
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi(mwenye miwani) akitoa   maelekezo  ya namna bora ya kufanya kazi katika kikundi kwa  wakikundi   cha Jitume Vijana chenye vijana kumi katika kijiji Ikungi, ambacho pia kilichopata mkopo wa shilingi milioni 25 kwa ajili ya mradi wa kutengeneza matofali ya sementi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.. Mkopo huo ni Mkakati iliyojiwekea Halmashauri ya Ikungi wa kudhibiti na kupambana na ugonjwa wa Covid-19 kwa kutoa mikopo hiyo isiyo na riba kwa vijana ili waweze kujitenga na kujifungia na kuendelea na uzalishaji  mifuko hiyo.Nyuma yake Kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Justice Kijazi, pembeni  kulia (mwenye koti jeusi) ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi(mwenye miwani) akipata maelekezo  kutoka kwa  katibu wa kikundi cha The New Bright Future - Petro Mwacha  jinsi mashine ya kutengenezea mifuko mbadala  ya kikundi cha The New Bright Future chenye vijana  10 waliopewa mkopo wa Milioni 25 na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mara  baada ya kuzindua kiwanda hicho. Mkopo huo  ni Mkakati iliyojiwekea Halmashauri ya Ikungi wa kudhibiti na kupambana na ugonjwa wa Covid-19 kwa kutoa mikopo hiyo isiyo na riba kwa vijana ili waweze kujitenga na kujifungia na kuendelea na uzalishaji  mifuko hiyo.Nyuma yake Kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Justice Kijazi, Kulia (mwenye koti jeusi) ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo

Mkuu wa Mkoa wa  Singida(mwenye Miwani) akiuliza  maswali kwa  vijana wanaotengeneza mifuko mbadala  ya kikundi cha The New Bright Future(mwenye koti jeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo, Nyuma ya Mkuu wa Mkoa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi

Na John Mapepele, Singida


Falsafa ya Rais John Pombe Magufuli ya kutaka wananchi wake kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na wataalam wa afya za kudhibiti na kujikinga na ugonjwa, wa Covid-19, kumwomba Mungu na kuendelea kuchapa kazi ili kunusuru kupoteza maisha na kushuka kwa uchumi wa nchi yao zimetekelezwa kwa vitendo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Akitekeleza falsafa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ikungi na kuzindua kiwanda cha kutengeneza mifuko mbadala katika Kijiji cha Siuyu Wilaya ya Ikungi.

Kiwanda hicho kilichoanzishwa kikundi cha New Bright Future chenye vijana 10 waliopata mkopo usio na riba wa shilingi milioni 25 na Mradi wa kutengeneza matofali ya sementi wa Kikundi cha Jitume Vijana chenye vijana 10 kwenye Kijiji Ikungi ambacho pia kimepata milioni 25 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Ikiwa ni mkakati maalum wa kupambana na gonjwa la Covid-19 kwa kuwatenga na kuwafungia vijana kwenye uzalishaji wa bidhaa badala ya kuzagaa katika mikusanyiko isiyo ya lazima inayoweza kusambaza ugonjwa huo kirahisi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi, hadi sasa tayari Halmashauri imeshatoa jumla ya milioni 127 kwa wanufaika 78 ambapo inatarajia kutoa hadi milioni 150 kwenye mwaka huu wa fedha endapo makusanyo yatakuwa kama yalivyokadiriwa



Dkt. Nchimbi amepongeza mikakati inayofanywa na Halmashauri ya Ikungi kwa ubunifu na uratibu mzuri wa kutoa na kuelekeza mikopo kwenye miradi ya viwanda vya uzalishaji bidhaa.

Ambapo amesema kwamba mkoa huo umeendelea kuweka mkakati wa kudumu wa kujitenga na kujifungia katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji ikiwa ni pamoja na viwandani ili kuepukana na kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19 na kuongeza uzalishaji unaoendana na falsafa ya Mhe. Rais Magufuli wa kuchapa kazi kwa bidii na kuendelea kuzingatia maelekezo ya wataalam katika kipindi hiki.

Ameitaka Halmashauri ya Ikungi kutatua changamoto zote zinazokikabili kikundi cha The New Bright Future ili kiweze kuzalisha kikamilifu na kisaidiwe kupata masoko ya uhakika wa bidhaa zake ili fedha ya Serikali iliyotolewa isipotee bali iwe na tija hatimaye iweze kurejeshwa na kuwanufaisha wakopaji wengine

Aidha amezielekeza Halmashauri zote katika Mkoa wa Singida kuiga mfano wa Halmashauri ya Ikungi katika utoaji wa mikopo inayoelekeza katika uzalishaji wa bidhaa na viwanda na kupiga marufuku kutoa mikopo ya fedha na kwamba mikopo lazima itolewe kwa kasi kama kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 ili wanavikundi hao wajitenge na kuendelea na uzalishaji

Akiwa kwenye Soko maarufu la viazi lishe kwenye Kitongoji cha Kideka katika Kijiji cha Nkunikana aliwapongeza wafanyabiashara hao kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa kuandaa miundombinu ya maji ili kunawa mikono kwa sabuni katika maji yanayotiririka wakati wote.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwataka wakulima wa viazi lishe kuendelea kulima kwa bidii ili wananchi wapate lishe bora kutokana na viazi hivyo na majani yake ambapo alisisitiza kuwa katika kipindi hiki ni muhimu kusanitaizi mikono na kusanitaizi afya zao

“Naelekeza wakulima waache visingizio nao waendelee kwenda mashambani kujitenga na kulima kwa bidii katika kipindi hiki ili waweze kupata mazao mengi na wakati huo huo watekeleze matakwa ya Serikali ya kujitenga na mikusanyiko isiyo ya lazima ambayo ingeweza kusababishia maambukizi endapo mmoja ana maambukizi.”



Dkt. Nchimbi amesema ugonjwa Covid-19 uwe ni chachu ya kufanya kazi kwa bidii za uzalishaji na kwamba viwanda hivyo viwe darasa maalum ya kutolea mafunzo hayo bila malipo kwa vijana wengine ili kuwapa maarifa kwa vijana wengi zaidi

Katika uzinduzi huo mkoa huo ulitoa kiasi cha shilingi milioni moja huku Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ikitoa kiasi cha shilingi milioni tano na kufanya jumla ya shilingi milioni 6 zilizoombwa na kikundi cha The New Bright Future kwa ajili ya kununua malighafi kupatikana.

Katika hatua nyengine Mkuu wa Mkoa alielekeza Serikali ya Wilaya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kutumia jengo jingine la Kijiji cha Isuna katika Wilaya ya Ikungi ambalo ni mali ya Serikali kwa vikundi vya uzalishaji ambalo kwa sasa halitumiki kwa shughuli yoyote ile.

Akisoma hotuba mbele ya Mkuu wa Mkoa Katibu wa kikundi cha The New Bright Future Petro Mwacha ameishukuru Serikali kwa kuwapa mkopo huo na kusisitiza kuwa mradi huu umelenga kuunga mkono juhudi na kauli mbiu za Rais, John Pombe Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo alisema Serikali ya Wilaya tayari imejipanga vizuri kujikinga na ugonjwa huo ambapo hadi sasa elimu ya ugonjwa wa Covid-19 kwenye maeneo mbalimbali inaendelea kutolewa.

Amesema Wilaya ya Ikungi ni miongoni mwa Wilaya ambazo zipo katikati ya nchi ya Tanzania ambapo barabara kuu inayounganisha mikoa na nchi mbalimbali na kwamba mwingiliano wa watu ni mkubwa, hivyo njia bora ya kukabiliana na ugonjwa huu ni wakuwatenga watu kwa kutumia mkakati maalum wa kuwapa mikopo ambayo itawafanya wananchi wajifungie na waendelee na uzalishaji huku wakichukua tahadhari zote za kujikinga zinazotolewa na wataalam wa afya.
Share:
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: