Saturday, 14 March 2020

RC Mnyeti awataka Wanasiasa wafanye kazi na kuacha kueneza chuki.

Na John Walter-Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amewataka viongozi wa Umma na wanasiasa kuacha tabia ya kueneza chuki hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la ushauri la mkoa,amesema jukumu lake kubwa ni kuhakikisha ulinzi na usalama kipindi cha uchaguzi.

Ameshauri kwa  kipindi kilichobaki wanasiasa na viongozi wafanye  kazi inayowapasa kwa kuwa  wenye jukumu la kuamua nani awe mwakilishi wao ni wapiga kura.

“Mimi ni kiongozi wa mkoa  siwezi kuingilia mchakato wa ndani ya chama”alisisitiza

“Imefika mahala ukienda msibani ukisalimiana na mtu matukio kama hayo yanahusishwa na siasa jambo ambalo si kweli” alisema Mnyeti.

No comments:

Post a Comment