Thursday, 20 February 2020

WAZIRI MKUU KESHO KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI KIGOMA


Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu wa ziara ya waziri mkuu inayoanza kesho Mkoani Kigoma

Na Editha Karlo,Kigoma

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuanza ziara ya siku mbili ya  kikazi na ya chama cha mapinduzi(CCM)Mkoani Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu Emanuel Maganga amewaeleza waandishi wa habari leo  kuwa waziri mkuu atawasili mkoani hapa kesho majira ya saa tatu na nusu asubuhi kwaajili ya shughuli maalum za chama cha mapinduzi(CCM)pamoja na shughuli zingine za kiserikali ikiwemo kupewa taarifa za Mkoa huo ambapo shughuli hizo zitafanyika siku ya kwanza ya ziara yake.

"Kama mnavyojua Waziri Mkuu ni mlezi wetu wa chama cha mapinduzi wa Mkoa wa Kigoma na Kagera atapata nafasi ya kuongea pia viongozi wa Mkoa wa chama hicho katika vikao vyao vya ndani"alisema

Maganga alisema siku ya pili ya ziara yake Waziri mkuu ataelekea kwenye kituo cha utafiti cha zao la michikichi katika eneo la kihinga kisha kufanya mkutano wa hadhara na wananchi katika  eneo la viwanja mwanga centre.

Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya waziri mkuu.

No comments:

Post a comment