Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Ripoti ya Fedha iliyowasilishwa juzi kwenye bunge la Afrika mashariki EALA imeonekana kuwa na mapungufu mengi ya ubadhirifu wa fedha kwenye maeneo mengi hali itakayopelekea kuwepo kwa mjadala moto bunge humo.

Akiongea nje ya ukumbi wa bunge hili mbunge wa bunge hilo Mhandisi Habibu Mnyaa alieleza kuwa wanaenda kuipitia ripoti hiyo ili kuijadili kwa kina maeneo mbali mbali yalionyesha uwepo wa ubadhirifu wa fedha.

Alisema kuwa maeneo ya manunuzi ya umma kwenye sekretariet ya jumuiya hiyo ni sehemu mojawapo iliyo na mapungufu licha ya kuelekeza kufanywiwa kazi kwenye kikao kilichopotia.

"Ngojeni tukaipitie Kwanza ripoti hii tutakuwa sawa kuiongelea wiki ijayo kwenye mjadala utakapoanza kwa Sasa sina mengi ya kuongea naenda kuiptia Ila majadala utakuwa moto Sana kwa maeneo mengi yameonyesha kuwa na mapungufu"Alisema Mnyaa

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi wa fedha ya bunge hilo  Dkt. Ngwaru Maghembe alieleza bunge hilo kuwepo kwa marudio ya ubadhirifu wa fedha kwenye maeneo ya manunuzi na uandaaji wa ripoti japo sio kama ilivyokuwepo kwa kipindi kilichopita.

Alisema kamati hiyo imebaini kuwepo kwa watumishi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa mikataba mifupi ya mwaka moja hadi miwili na kujikuta sheria za kazi zikiwataka kuajiriwa jambo ambalo wanashauri kuona waajiriwa wanaajiriwa kwa taratibu kanuni na sheria za kazi.

"Tumebaini wahasibu wengi hawajapewa mikataba ya ajira za moja kwa moja wengi wamepewa mikataba ya miaka miwili na halafu wanaongezewa na hao wengi ni wa hapa nchini jambo hilo tumeelekeza wafuate taratibu za ajira"

Anabainisha kwamba ripoti ya mwaka huu imeonyesha kuwa jumuiya imepata hati safi japo Kuna changamoto kadhaa ambazo tumeelekeza kufanyiwa kazi kuondoa changamoto hizo kwa lengo la kuendelea kufanya vizuri.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: