NA HERI SHAABAN

KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Kipawa Mtaa wa Mogo  wilayani Ilala wamesheherekea Miaka 43 ya kuzaliwa kwa CCM kwa kufanya ziara kuangalia mradi wa Reli ya Kisasa ambao umepita eneo hilo.

Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mogo George Mtambalike na Mwenyekiti wa CCM  Said Mkuwa na Maofisa wa Shirika la Reli TRC.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mogo George Mtambalike alipongeza mradi wa reli ya kisasa na kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano.

Mtambalike alisema kupita kwa mradi huo Mtaa wa Mogo imefanya eneo hilo kukua katika shughuli za uzalishaji  uchumi   na thamani ya vitu kupanda bei.

"Mradi huu wa Reli ya kisasa mzuri sana tunaunga mkono utekelezaji wa Ilani ya CCM inayoongozwa na Mwenyekiti wetu Rais John Magufuli ambaye anatekeleza kwa vitendo sambamba na miradi mkakati ambayo ipo katika wilaya yetu ya Ilala " alisema Mtambalike.

Aidha Mtambalike aliwashauri Shirika la Reli TRC waweke kituo cha kushusha abiria Kipawa abiria wa kutoka Bara kwa ajili ya kuwaondolea usumbufu wananchi kushuka stesheni.


 Alisema dhumuni la ziara hiyo kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama na  kukagua miradi ya maendeleo.

Alisema katika mafanikio changamoto azikosekani  ameomba  TRC waboreshe miundombinu na njia za mifereji ili kuruhusu maji kupita yasilete madhara kwa wananchi wake kutokana na maeneo mengine kuziba na kuleta mafuriko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mogo Said Mkuwa alisema katika kuadhimisha kuzaliwa kwa chama wanajishughulisha katika shughuli za Jamii ndani ya mtaa huo na kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli  sambamba na kushiriki katika kuboresha mazingira ili mtaa uweze kuwa msafi.

Naye Mhandisi wa Shirika la Reli TRC Simon Mbaga alisema maombi ya kujenga kituo Kipawa cha abiria kutoka Bara wameyapokea watayafanyia kazi.

Mmbaga pia alielezea mradi wa reli ya kisasa amesema ujenzi wake umefikia asilimia 70 mafundi wanaendelea na ujenzi.

Amewataka wananchi wasikae Katika miundombinu ya reli na kusambaza kokoto  watakaokutwa wakifanya uharibifu watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: