Monday, 30 December 2019

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AWASILI MKOANI TANGA KWA MAPUMZIKO YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA

Leo Desemba 30/2019 Tanga Airport  tumempokea Mhe.Benjamin William  Mkapa, Rais mstaafu awamu ya tatu  ambaye amekuja nyumbani kusherehekea nasi mwaka mpya.

Mapokezi yameongozwa na Mhe.DC wilaya ya Muheza  , na kuhudhuriwa na  Kamati ya ulinzi na usalama mkoa na wilaya ya Tanga,  Kaimu Mkurugenzi Jiji la Tanga Ndg. Poss,  Mhe. Mkoba Mwenyekiti ccm wilaya,Ndg. Kidima Katibu ccm wilaya na Ndg. Kapange Katibu siasa na  uenezi  wilaya pamoja na wakuu was idara za serikali.

Lupakisyo Kapange
Katibu Siasa na Uenezi
Wilaya ya Tanga
Rais mstaafu wa awamu ya tatu,Mhe.Benjamini William Mkapa akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanaasha Tumbo mara baada ya kuwasili leo katika Uwanja wa Ndege mkoani Tanga.


No comments:

Post a comment