Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ngazi ya Mkoa na Wilaya kuwahoji watumishi wawili, Afisa Manunuzi na Mhandisi wa Majengo wa Wilaya ya Ulanga kwa tuhuma ya kutosimamia ipasavyo fedha zaidi ya shilingi 400 Mil. zilizoletwa Wilayani humo kwa ajili ya kuboresha Hospitali ya Wilaya hiyo.

Ole Sanare ametoa agizo alipotembelea ujenzi wa jengo litakalotumika kama Wodi ya akinamama ikiwa ni moja kati ya majengo manne yaliyopelekewa fedha hizo kwa lengo la kuboresha huduma ya Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Ulanga.

Akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa huyo alifika kukagua ujenzi wa jengo hilo ambalo liko katika hatua ya upauaji na kukuta mbao zinazotumika kuezeka hazina kiwango na hazijawekewa dawa ya kuzuia wadudu wahalibifu (Treated). Baada ya mahojiano ya muda ikaonekana kuna kila dalili ya mbazo zinazotumika katika jingo hilo hazikidhi vigezo vya BOQ hivyo kuagiza TAKUKURU kuwachunguza watumishi hao,
“hakuna kucheza, fedha zimeletwa kwa ajili ya kuwahudumia watu wa Ulanga, usihangaike kutemba na hizo fedha, utatapika” alionya Ole Sanare.

Aidha, Ole Sanare amesema hata kama itadhibitika hawakutumia hizo fedha za mradi huo kwa maslahi yao binafsi lakini kama wataalamu bado wana kosa la kutosimamia ipasavyo matumizi ya fedha hiyo ya Serikali hivyo ni lazima wawajibike.

“Chunguzeni pelekeni mahakamani,Mkurugenzi wakiwepo mahakamani anzeni process hatua nyingine ziandaliwe hatua za kinidhamu ukitoka unalo”
Mkuu wa Mkoa pia anatumia fursa hiyo ya kujitambulisha kufuatilia Maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa aliyoyatoa wakati wa ziata yake Mkoani Morogoro Mwezi Septemba mwaka huu.

Amesema kwa kiasi fulani baadhi ya maagizo yaliyotolewa na kiongozi huyo yametekelezwa lakini akataka kuongeza kasi kwa yale ambayo hayajatekelezwa huku akiagiza watumishi nane wanaotuhumiwa kufanya ubadhilifu wa fedha za Halmashauri hiyo zaidi ya shilingi 1.4 Bil, kufikishwa mahakamani haraka na wale wanaojaribu kutoroka wakamatwe mara moja.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama kumfikisha mahakamani Diwani Kesy Mponda Wilayani humo anayetuhumiwa kukaidi kurudisha fedha za Serikali alizochukua kwa ajili ya kwenda kwenye ziara ya majifunzo ya Kilimo kwenye Maonesho ya Nanenane Mjini Morogoro mwaka huu 2019 pamoja na Madiwani wenzake lakini alishindwa kushiriki mafunzo hayo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: