Na. Catherine Sungura-Morogoro

Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kimetakiwa kuweka msisitizo kwenye masuala ya utoaji elimu kuhusiana na chanjo nchini ili  idadi ya watoto wanaopatiwa chanjo kufikiwa.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa chama cha Madaktari Wanawake Tanzania  ambao unafanyika mkoani hapa.

Dkt. Magembe amesema kuwa elimu ya afya kwa wananchi inatakiwa kushushwa hadi chini ili taarifa kuweza kuwafikia walengwa wengi na hivyo kuweze kufika kwenye vituo vya afya kupata chanjo ili kuwakinga watoto katika  hatari ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. 
"Suala la chanjo ni la kuwekea msisitizo hivyo endapo tutashirikiana katika utoaji wa elimu hususan pale wizara inapokuwa na kampeni za chanjo ili watoto wetu wachanjwe na  kufikia adhima ya serikali ya kuwa na watoto waliokingwa kwa chanjo inatimia”.

Hata hivyo amekishukuru chama hicho kwa kutoa huduma za afya kwa upande wa wanawake hususani saratani ya mlango wa kizazi na ile ya matiti

“Wanawake ni taifa kubwa na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ni uchumi wa kati kupitia  viwanda hivyo hatuwezi kuwa na uchumi wa kati endapo wananchi wake ni wagonjwa hususani wanawake ambao ni wazalishaji” Alisisitiza Dkt. Magembe.

“Serikali inatambua mchango wengu MEWATA kwa upande wa saratani kwa miaka mingi hivyo imeweza kujenga vituo vya kutolea huduma zaidi ya mia nne na katika hivyo asilimia sabini ni vituo vya afya ambavyo vinatoa huduma ya upasuaji nchini yote inatokana na mchango wenu kwani mlipita nchi nzima kuwasaidia wanawake licha ya mazingira yaliyokuwepo”. 

Hata hivyo alisema hivi sasa magonjwa yasiyoambukiza  yanachangia asilimia arobaini ya vifo nchini hivyo serikali  kupitia wizara ya afya ilifanya tathimini ya sera ya afya na kuona magonjwa hayo yanaongezeka kwa kasi  na kuua watu wengi na kisababishi kikubwa  ni mtindo wa maisha pamoja na vyakula 

“kwa kuona hili kama wizara imekuja na mpango wa taifa wa magonjwa yasiyoambukizwa ili kila mdau aweze kuunganisha nguvu katika kupambana na magonjwa haya”.

Aidha, alibainisha kuwa  saratani ya mlango wa kizazi ni kati ya magonjwa  yanayoongoza kusababisha vifo kwa wanawake kwa takribani asilimia hamsini ya wanawake wote wanaoonwa na  saratani ya mlango wa kizazi inaongoza  ikifuatiwa na saratani ya matiti.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo amewata MEWATA kutafuta namna  ya kushughulika na vitendo vya unyanyasaji  na ukatili wa kijinsia kwa watoto wadogo na wanawake kwani vitendo hivyo sasa hivi vimekua vikiongezeka kila siku,

 na hivyo kukitaka chama hicho kutoa elimu kwa jamii ili kuondoa vitendo hivyo kwa kuhakikisha inazungumza na jamii kuhusu suala la ukatili kwa watoto kwani hivi sasa watoto hawako salama na wanaathirika kisaikolojia na endapo jamii haitashiri katika malezi ya watoto jamii haitokuwa vizuri miaka ijayo.

-Mwisho-
Share To:

msumbanews

Post A Comment: