Friday, 8 November 2019

Ilala imetenga milioni 800/= kwa ajili ya jengo la Halmashauri


NA HERI SHAABAN(ARNATOGLOU)

HALMASHAURI ya Ilala imetenga jumla ya shilingi milioni 800/= katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020  kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmashauri ya Ilala.


Akizungumza katika  Baraza la Madiwani manispaa ya Ilala leo Mkurugenzi wa Ilala Jumanne Shauri alisema  jengo hilo litajengwa  gholofa kumi ambalo litatumika na watumishi wa manispaa ya Ilala.

Mkurugenzi Jumanne Shauri alisema kwa sasa halmashauri ipo katika Mchakato wa kumtafuta Mkandarasi atakayesanifu na kusimamia ujenzi wa Ofisi kisha Mzabuni kutafuta Mkandarasi ujenzi utatangazwa rasmi.

Alisema baada kikao cha madiwani kupitisha tayari wataendelea na mchakato mwingine.

Kwa upande wake Meya wa halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto alisema HOSPITALI ya​ plani iliyopo Buguruni kwa Mnyamani imeanza kutoa huduma ya upasuaji kwa wajawazito bure kuanzia Novemba mwaka  2019

Meya wa Ilala Kumbilamoto   alisema hayo kwenye kikao Cha baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala kupitisha miradi ya maendeleo katika kipindi Cha robo ya kwanza ya mwaka.

Alisema kuwa huduma hiyo imeanza kutolewa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo manne ya hospitali hiyo.

Aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano ilitoa jumla ya milioni​ 500 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la upasuaji na kwa Sasa limekamilika.

Pia alisema wamepokea vifaa vya kisasa vya upasuaji ambapo vinathamani ya jumla ya shilingi milioni 177ambavyo vimeanza kutumika.

"Huduma ya upasuaji kwa​ wajawazito katika hospitali hiyo ni bure hakuna atakayetozwa fedha na kujifungua ni bure"alisema Kumbi lamoto.

Aliongeza kuwa halmashauri ya ilala itatoa jumla ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya jengo la mama na mtoto katika hospitali hiyo.

Alisema hospitali ya Amana kujifungua kwa njia ya kawaida Ni shilingi 75000/= kwa upasuaji Ni shilingi 25,0000/=kwa  Sasa.


No comments:

Post a comment