Sunday, 27 October 2019

Malengo 17 Ya UN Kupelekwa Mlima Killimanjaro


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Vijana wa Kiafrika kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamejipanga kupanda Mlima Killimanjaro kwa lengo la kuhamasisha vijana kushiriki katika kutimiza Malengo endelevu ya  Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UN) ambapo watakuwa vijana wa kwanza kupeleka bango la malengo hayo katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Mratibu wa Mpango huo Munyaradzi  Muzenda kutoka nchini Zimbambwe anasema kuwa wanaendesha kampeni ya Mlima Kilimanjaro ishi ndoto zako ambayo inalenga kuhasisha malengo endelevu ya UN pamoja na kuhamasisha malengo  Umoja wa Afrika 263 ya Afrika tunayoitaka.

Munyaradzi anasema kuwa  jumla ya vijana 17 watapanda na vibao vya malengo hayo wakijikita zaidi kwenye lengo namba moja la Kupondoa Umasikini na kuhimiza vijana kushiriki katika shughuli zitakazosaidia kutokomeza umasikini.

Aidha amesema kuwa Tanzania itakua nchi ya kwanza duniani kupeleka malengo hayo katika mlima huo wa pili kwa urefu duniani hivyo amewataka wadau kuungana katika kampeni hiyo ya kupanda mlima mwishoni mwaka huu.

“Vijana kutoka mataifa mbalimbali watafika Arusha kwa ajili ya kupanda mlima na tunatarajia kampeni hiyo itafanikiwa kwa kiasi kikubwa” Alisema Munyaradzi


No comments:

Post a Comment