Mratibu wa Kongamano la kuombea nchi amani kutoka Taasisi ya Mudir Markaz Safina, Sheikh Said Kinyogoli(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano hilo mjini hapa jana.Kulia ni Sheikh Najim Humoud na kushoto ni Imamu Sheikh Abubakar Masuala. (Picha Boniphace Jilili).


Na Boniphace Jilili, Singida 

Kongamano kubwa la kuiombea nchi amani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika mkoani Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Mratibu wa Kongamano hilo Sheikh Said  Kinyogoli alisema limeandaliwa na TaasAsi ya Mudir Markaz Safina chini ya baraza kuu la waislam Tanzania (Bakwata),lengo likiwa ni kuiombea nchi amani katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

"Panapo kusekana amani hauwezi kufanya jambo lolote liwe la kijamii na la kimaendeleo kwani ukijaribu mara unasikia bomu linalipuka kwasababu hakuna amani." alisema Sheikh Kinyogoli.

Sheikh Kinyogoli alisema kongamano hilo litafanyika kwa siku saba katika viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi mjini hapa, kuanzia siku ya jumatano wiki hii na litashirikisha watu wote bila kujali itikadi za kidini, ambapo watakuwepo masheikh, Hilary Kipozeo, Hashim Mbonde na Mzee Yusuph wote kutoka Dar es salaam. 

Wengine ni Sheikh Jafari Abdulahaman kutoka Morogoro, Sheikh Mohamed Makarani-Mwanza pamoja na Sheikh Ibrahim Mlumbango kutoka Kigoma. 

Alisema sanjari na kuiombea nchi amani pia watakuwa wanaadhimisha mwaka mpya wa kiislam ambapo watatoa nasaha za kidini ili watu wawe na hofu ya Mungu.

Sheikh Juma aliongeza kuwa katika kongamano hilo yatatolewa mafunzo ya ujasiriamali kwa ajili ya watu kujifunza mbinu za kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji ili kujiinua kiuchumi. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: