Na Alphonce Kusaga, Arusha

Mdau wa Soka nchini, Dkt Athumani Kihamia ametoa ushauri wake kwa TFF na  sababu saba za kushindwa vibaya kwa Timu ya taifa Stars Kushindwa mashindano ya Afcon 2019.

Akizungumza na Muungwana Blog  Kihamia amesema sababu moja wapo kuwa uteuzi wa wachezaji haukuzingatia uhalisia kwa kuwa wachezaji waliofanya vizuri kwenye ligi ya ndani hawakujumuishwa.

Kihamia amesema kuwa mfano wachezaji waliachwa mfano Mkude ambaye ni Kiungo cha Kukaba,pamoja na Ajibu upande wa Pasi za Mwisho ambao uliiponza Tanzania kwenye eneo hilo na Taifa kushindwa kufunga Magoli.

Sababu ya Pili Kihamia amesema kuwa ni kutokuwepo kwa bodi ya ligi inayoaminika ambayo imechangia kubadili ratiba ya ligi mara kwa mara kutokana na misingi ya utashi na kukosekana kwa weledi.

Ameongeza kuwa hali hiyo imesababisha kuwepo kwa msimamo wa ligi usiokuwa na uhalisia hivyo kufanya wachezaji kutokuwa na utimamu wa mwili endelevu unaowaimarisha katika mashindano.

Akizungumzia suala la tatu ambalo ni kukosa wadhamini Kihamia amesema hali hiyo imesababisha kutokuwepo kwa mazingira sawa miongoni mwa washindani ambao ni vilabu ambapo matokeo yake msimamo wa ligi hauakisi hali halisi ya ubora wa Timu.

Suala la Nne amesema waamuzi wa Ligi kuu wameonekana wazi baadhi wakizibeba baadhi ya Timu na kukandamiza wengine huku bodi ya ligi ikifumba macho na masikio ya wadau wake wakuu wanapolalamika na kujikita zaidi kwenye kupangua ratiba bila ulazima na kutoangalia athari za kiuchumi na kisaikolojia kwa Timu.

Sababu ya tano Dkt Kihamia amesema kuwa waandishi wa habari walitumia muda mwingi kwa kalamu zao kuipamba taifa stars kwa sifa ambazo hawana na ambazo hawajazifikia.

Uongozi wa Timu ya Taifa Kihamia amesema ni miongoni mwa sababu ya sita ambapo uongozi ulipo umekosa mchanganyiko ambao unabeba taswira ya taifa badala ya uliopo ambao unaonyesha wasanii na viongozi wachache ambapo wapo Dar es salaam Peke yake.

Hata hivyo katika sababu ya saba ametoa maoni yake kuwa ni vyema TFF ikaweka nguvu kubwa kwa vijana wa U23,U20 na U17 pamoja kurejeshwa kwa mashindano ya mikoa ambapo yataleta hamasa kubwa kupata wachezaji wenye vipaji kwa njia rahisi huku Serikali ikiimarisha mashinsano ya shule za Msingi na Sekondari.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: