Tuesday, 21 May 2019

EWURA CCC YATOA ELIMU KWA ZAIDI YA WANAFUNZI 70 KWA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA TAWI LA ARUSHA.

 Getrudi Mbilingi Afisa Utawala na Utumishi Ewura CCC Makao Makuu Dar es salaam akitoa ufafanuzi kuhusiana na haki ya mtumiaji wa Nishati na Maji.
 Lukingo Lukingo Afisa Menejimenti na Huduma kwa Wateja Ewura CCC akiwa anatoa ufafanuzi kuhusiana na kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo ya serikali.
Said Mremi Afisa Uhusiano Tanesco Mkoani Arusha ;ni lazima mteja anapoluja kuomba kuunganishiwa umeme wakati anajaza fomu ya maombi lazima ajaze kwa usahihi,ahainishe idadi ya vifaa ambavyo anahitaji kuvitumia ili ikitokea hitilafu shirika liweze kuona namna ya kulipa fidia kwa mteja huyo
Jennifer Daniel Katibu wa kamati ya watumiaji huduma ya mkoa wa Arusha  (RCC) akiwasilisha mada kwa wanafunzi wa Chuo kikuu huria Nchini Tanzania tawi la Arusha  namna ya kutoa malalamiko kwa njia sahihi ili mteja aweze kulipwa stahiki zake 

 Dkt.Peter Kashingo Mwenyekiti RCC Mkoani Arusha.Aizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu huria nchini Ranzania tawi la Arusha 
baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya kiserikali ya EWURA CCC mkoa wa Arusha iliyowajumuisha wanafunzi wa Chuo kikuu huria Tanzania tawi la Arusha 
Gerald sambayuka Mjumbe wa kamati ya watumiaji wa mkoa ambayo ipo chini ya EWURA CCC mkoani Arusha
Washiriki wa semina kutoka Chuo kikuu huria nchini Tanzania tawi la Arusha wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali  zinazowasilishwa katika mafunzo yaliyoandandiliwa na Baraza la uUshauri la watuamiaji wa huduma ya a Nishati na Maji  Ewura CCC 
Injinia Raymond David ambae ni Mhazini wa RCC Arusha akitoa ufafanuzi wa sheria kwa watumiaji wa wa huduma za Nishati na Maji .
 Getrudi Mbilingi Afisa Utawala na Utumishi Ewura CCC Makao Makuu Dar es salaam akitoa ufafanuzi kuhusiana na haki ya mtumiaji wa Nishati na Maji.
 Kutoka katikati ni Lugiko Lugiko Afisa Menejimenti na Huduma kwa wateja  Ewura CCC Jijini Arusha,wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ewura CCC Dkt.Peter Kashingo,kulia kwake ni Mhazini wa RCC Arusha Raymond David,Kutoka kulia ni Jennifer Daniel Katibu RCC Arusha,kulia kwake ni Gerald sambayuka Mjumbe wa kamati ya watumiaji wa mkoa ambayo ipo chini ya EWURA CCC mkoani Arusha

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Baraza la uUshauri la watuamiaji wa huduma ya a Nishati na Maji  EwuraCCC  imeendesha programu ya mafunzo kwa wanafunzi zaidi ya sabini wa Chuo Kikuu Huria Tanzania katika tawi la Arusha.

Lukingo Lugiko ni Afisa Menejimenti na Huduma kwa wateja Ewura CCC amesema semina hiyo ni sehemu ya uelimishaji ambazo wanalenga kuifikia jamii ya watanzania hususani watumiaji wa huduma za Nishati na Maji.             

Lukingo amesema  lengo kubwa   ninkuwafundisha watumiaji wa huduma hizo kuzitambua haki zao kwani watu wengi hawajui haki na wajibu wao kama walaji.  

 "Watanzania wengi wanatabia ya kunung'unika badala ya kulalamika kwa maandishi ili wahusika waweze kutatua matatizo yao yananyowakabili wao kama walaji" alisema Lugingo

Getrudi Mbilingi Afisa Utawala na Utumishi Ewura CCC Makao Makuu Dar es salaam akitoa ufafanuzi kuhusiana na haki ya mtumiaji wa Nishati na Maji amesema kuwa taasisi inayo dawati kwa uelimishaji kwa umma kuhakikisa taarifa zinafika kwa kushirikiana na watoa huduma na watendaji wa serikali za vijiji na mitaa ammbao wanafanya nao kazi kwa ukaribu

Said Mremi ni Afisa uhusiano kutoka Tanesco ambaye alimuwakilisha meneja amesema kuwa mteja kabla ya kuomba kunganishwiwa huduma ya umeme ni vyema akajaza fomu kwa usahihi sambamba na idadi ya vifaa amabavyo mteja atavitumia ili tatizo litakapotokea iwe rahisi kutatuliwa au kupewa fidia kwa mteja husika.

"Kama mteja ana madai ya fidia anayohisi yamesababishwa na tanesco swala la utaratibu la ulipaji wa fidia tanesco wanadawati la fidia,vyema mteja husika alete malalamiko yake kwa maandishi na awe na uhakika kwamba anachokileta ni kile alichokijaza kwenye fomu maana kuna baadhi ya wateja ni waongo na wanataja taarifa za uongo"alisema Mremi

 Akijibu swali la mmoja wa washiriki wa semina hiyo kuhusiana na tatizo la kukatikakatika kwa umeme na kwanini tanesco hawalipi fidia Mremi amesema kuwa yapo matatizo ya umeme ambayo tanesco wananyapanga na wanatoa taarifa kwa wateja wao, matatizo mengine yanatokea kwa dharura siyo kwa kupanga ambayo yapo nje ya uwezo wa Tanesco.

"Mfano limepita gari lina vyuma likakata nyaya na umeme ukakatika,mtu amekata mti huko ukaangukia nyaya umeme ukakatika huwezi kuja kuidai tanesco kisa samaki zako zimeharibika,mtu amegonga nguzo akakimbia wananchi wamechelewa kutoa taarifa hilo halowezi kuwa kosa letu hilo ni tatizo la umeme la dharura" alisema Mremi

Dkt.Peter Kashingo ni Mwenyekiti wa kamati ya RCC mkoa amesema  kutumia teknolojia mpya ambayo inaweza kupunguza matumizi ya umeme majumbani kutoka 50%-70% kwa kuthibiti muda ambao taa huwaka bila sababu za msingi.

"Utumiaji wako mzuri wa huduma ya umeme ni moja ya njia sahihi ya haraka za kupungiza bili yako ya Nishati." Alisema Dkt.Peter Kashingo.

Injinia Raymond David ni Mhazini wa Ewura RCC ambapo amesema kuwa mtoa huduma anatakiwa kuhakikisha hatuabanazochukua dhidi ya mteja aliyeshindwa kulipa bili ni sahihi na siyo za kibaguzi

"Hakuna mteja atakayekatiwa huduma kama notisi ya siku 30 haijatolewa" alisema Raymond.

Ewura CCC ni Taasisi ya Kiserikali iliyoanzishwa kwa lengo ka kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa Nishati na Maji katika sura 414 ya sheria ya Ewura kifungu cha 30

No comments:

Post a comment