Saturday, 27 April 2019

MCHUNGAJI LWAKATARE AVUNJA NGOME ZA CHADEMA KILOMBEROMbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Kanda ya Kilombero Mh Mchungaji Mama Dr Gertrude Lwakatare Leo Tarehe 27 April 2019 Amefanya Ziara Ya Ufunguzi wa Mashina ya CCM Katika Kata Tisa za Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilaya ya Kilombero.

Ambapo Katika Ziara Hiyo Aliambatana na Kamati ya Siasa Ya Mkoa wa Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Ndugu Innocent Kalogeris.

Mwenyekiti Mwenyeji Wilaya Ya Kilombero Ndugu Clarance Mgomba Pamoja na Kamati ya Siasa Wilaya ya Kilombero.

Mh Mbunge wa Viti Maalum Gertrude Lwakatare Amefungua Mashina Matano Yakiwemo Shina la Saba Saba Kata ya Katindiuka, Shina la Vijana UVCCM Mchangani Kata ya Mlabani, Shina la Wakereketwa wa CCM Kiungani Kata ya Ifakara Mjini, Shina la Vijana Mangwale B, Kata ya Ifakara Mjini na Shina la Wakereketwa la Minalani Kata ya Viwanja Sitini Ifakara.

Katika Ziara Hiyo na Ufunguzi wa Mashina Hayo Pia Wanachama na Wakereketwa wa Vyama Vya Upinzani Wamerudi Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mashina Hayo Mh Lwakatare Amewataka Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Kuyatumia Mashina Hayo Kujenga Umoja, Mshikamano, Upendo na Kujiletea Maendeleo.

Pia Ameelezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020 Wilaya ya Kilombero na Kazi Nzuri Ya Rais Dkt.John Magufuli Anayoifanya ikiwemo Ujenzi wa Daraja la Kilombero, Elimu Bure, ujenzi wa Barabara ya Kidatu - Ifakara, Ujenzi wa Vituo Vya Afya na Ukusanyaji wa Mapato kwa Wingi.

Mh Mbunge Lwakatare Pia Leo atafanya Mkutano Mkubwa wa Kuzungumza na Wananchi Katika Stendi kwa Makali Ifakara Mjini Kuelezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM Katika Wilaya Ya Kilombero.No comments:

Post a comment