Thursday, 21 March 2019

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIFUMO YA MAJITAKA ILI KUEPUKA MAGONJWA YA MLIPUKO

Mkurugenzi wa Usimamizi huduma za MajiTaka wa DAWASA, Shabani Mkwanywe (kulia) akizungumza na wanahabari katika Wiki ya Maji Duniani inayoadhimishwa na DAWASA kwa kusikiliza kero za wananchi katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam iliyoanza Machi 16-22, 2019.
Mkurugenzi wa Usimamizi huduma za MajiTaka wa DAWASA, Shabani Mkwanywe (kushoto) akieleza machache mbele ya wanahabari juu ya mifumo ya MajiTaka
 Watoa Huduma wakiendelea kutoa elimu na kutatua kero za wananchi waliofika katika Wiki ya Maji Duniani inayoadhimishwa na DAWASA kwa kusikiliza kero za wananchi katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam iliyoanza Machi 16-22, 2019.

Wananchi wakisoma vipeperushi.


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) inatarajia kujenga miradi 50 ya jamii ya kuchakata majitaka katika maeneo yasiyopangwa ili kutatua changamoto za unyonyaji maji ikiwemo kuzuia magonjwa ya mlipuko.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Usimamizi huduma za MajiTaka, Shabani Mkwanywe amesema miradi hiyo ya jamii itajengwa katika maeneo ambayo huwa inakumbwa na magonjwa ya mlipuko.

Amesema pia kutajengwa vituo 25 vya kusafirishia MajiTaka kwa maeneo ambayo hayawezi kufikiwa kirahisi.

"Miradi hii itawasaidia kujibu changamoto za wakazi asilimia 70 kwa wanaotumia vyoo vya shimo na asilimia 20 vyoo vya matenki," amesema Mkwanywe. DAWASA inabuni miradi hiyo ikiwa wanasubiri kuanza kwa miradi mikubwa mitatu ambayo ni ile wa Jangwani, Kurasini na Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Amesema Changamoto kuwa inayowakabili ni Mifumo mingi ya majiTaka ilijengwa miaka 50 na 70 na Dar es Salaam haikuwa na watu wengi kama ulivyokwa sasa... wananchi wanatupa TakaNgumu na kusababisha kuziba.

Ameongeza kuwa ili kukabiliana na wananchi kukosa huduma ya majiTaka, DAWASA wamejipanga kununua malori ili kuweza kusaidia wananchi kupita mtaani na kukusanya kwa bei watakayoweza kuimudu tofauti na sasa huduma hiyo imekuwa ikitolewa na watu binafsi kwa gharama ya juu. --

Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

No comments:

Post a comment