Thursday, 21 March 2019

MKUU WA WILAYA AWAOMBA WADAU WA ELIMU KUMUUNGA MKONO KATIKA KAMPENI YA TOKOMEZA ZERO KISARAWE

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokete Mwegelo akizindua kampeni ya '' Tokomeza zero kisarawe '' wilayani hapo

Na. Vero Ignatus.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokete Mwegelo ameitaja kampeni ya Tokomeza zero kisarawe kuwa ni kampeni maalum kwa ajili ya kuongeza ufaulu na kuondoa kabisa zero wilaya ya kisarawe mkoa wa Pwani. 

Mhe. Jokate amesema wanaelewa kuwa changamoto wanazopitia waalimu na wanafunzi ni nyingi na wanaelewa kuwa Elimu ndiyo ufunguo wa maisha hivyo wanakisarawe wameona ni vyema kuwekeza katika Elimu. 

Ukimsaidia mtoto akaweza kupata elimu unakuwa umeweza kusaidia Tanzania nzima,na mimi kuanzia sasa nataka tuanze  na kidato cha nne na sita tufute hizo zero na zisiwepo kabisa. Katika kuhakikisha hii linatimia kuna mambo mengi ambayo tutafanya kwa kushirikiana na wadau wote wa elimu nchini. Alisema Joketi

Amesema mwaka 2017 kulikuwa na kammpeni ya Ondoa Zero ambayo ilifanikiwa  kupunguza zero kutoka 455 hadi 259 kwa kidato cha Nne na cha sita, pia mwaka jana waliweza kuwakusanya na kuwaweka kambini wanafunzi kwa pamoja na kuongeza ufaulu zaidi tofauti na awali

'' Kwa kuona hilo mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alizindua Kampeni dada ijulikanayo kama Tokomeza Zero Kisarawe ikijumuisha wanafunzi kuwekwa kwenye kambi kwa ajili ya massive training uboreshwaji wa miundo mbinu mashuleni na pia Elimu na kozi kwa waalimu ili kuinua kiwango cha Elimu wilaya ya kisarawe
Tuna lengo la kuongeza idadi ya vijana wanaongia vyuo vya kati na vikuu''

Kulingana na Utafiti unaonyesha wanafunzi wengi wa kisarawe hutembea umbali mrefu  kwenda shule  kwa zaodi ya km 15 kwenda pekee, hali ambayo inayofanya wanafunzi kufika shuleni wakiwa wamechoka. 

Miundo mbinu ya shule zetu ni changamoto sana n ahata Idadi za shule Wilayan ni chache ,tuna shule chache na kwa kulitambua hilo sisi tutashirikiana na wadau wa Elimu ili kuwezesha ujenzi wa shule kwa ajili ya wana kisarawe

Amesemankwa sasa wameamua kuweka. mkazo zaidi katika kampeni ya TOKOMEZA ZERO kuwa Wanafunzi wote wa kisarawe wa kidato cha nne na cha sita watapata mafunzo ya ziada ili kujiandaa na mitihani yao ya taifa, ili kuwaepusha na kazi za kila mara ambapo wanafunzi hao watakuwa kwenye kambi maaum kwa muda miezi miwili kabla ya muda wa mitihani yao ya taifa.

'' Tunawapatia waalimu mahitaji yote muhimu ili kufanikisha zoezi lao la ufundishaji na pia kuboresha miundo mbinu ya shule ili kuweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi na walimu"

Mhe. Joket amesema wanachokifanya kwa sasa katika  kuhakikisha tunafanikisha jambo hilo wameandaa Dinner Gala tarehe 30/03/2019 katika jitihada za kukusanya fedha ambazo zitatumika katika ujenzi ya Bweni, shule ambayo itakuwa na madarasa ya kutosha, maktaba pamoja na maabara zakisasa ambapo Shule hiyo  itakuwa ya kwanza ya aina yake kisarawe. 

Ameomba kwa akisema Mdau wa Elimu unaweza kushiriki kwa kuchangia 100,000 moja au kununua meza moja kwa shilling million moja ambapo hela zote hizo zitaelekezwa katika ujenzi wa shule hiyo ya kwanza ya aina yake yenye lengo la kuwa shule ya mfano ambapo shule zitakazofuatia zitaundwa kwa mfano  huo. 

Unaweza kushiriki kwa kuwasiliana nasi kwa namba hii ili kupata ticket yako 0677062070 au 0656132676No comments:

Post a comment