Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa mara ya kwanza kesho atapokelewa jimboni kwake, Monduli kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza uamuzi wake wa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo alitimkia CHADEMA mwaka 2015 na mwaka huu akaamua kurejea tena CCM.

Hapo kesho Machi 9, 209 Lowassa atafika Ofisi ndogo za CCM wilaya ya Monduli kama ishara ya kurejea rasmi nyumbani.

Utakumbuka Edward Lowassa alijiunga CHADEMA Julai 2015 baada ya jina lake kuenguliwa kwenye mchakato wa kutafuta mgombea wa urais ndani ya CCM.

Lowassa alitangaza kurejea CCM Machi Mosiukatika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais John Magufuli.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: