Wednesday, 1 August 2018

Msanii atakayekwenda nje bila kibali chetu faini mil.1 au kufutiwa usajili wake BASATABaraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeeleza wazi juu ya sheria zao na kanuni mpya ambazo zinawataka wasanii wote watakaokwenda nje ya nchi kwa lengo la kufanya show kuwa na kibali maalumu kutoka kwao kitakachomruhusu kufanya hivyo.

Akizungumza na wandishi wa habari Kaimu Katibu Mtendaji BASATA, Onesmo Kayanda amesema kuwa sheria hiyo ipo wazi isipokuwa wasanii wakubwa huwa hawahudhurii kwenye semina na midahalo pia hawasomi sheria za BASATA ndio maana wanataharuki linapotokea suala la utekelezaji.


Akizungumzia suala la faini juu ya kibali hicho, Kayanda amesema kuwa endapo msanii atafanya show nje ya nchi bila kibali kwa mara ya kwanza ataonywa na kutozwa milioni 1 na akirudia tena faini itaongezeka na ikiendelea tabia hiyo basi atafutiwa usajili wake.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: