Wednesday, 18 July 2018

WARAKA WA GIGY MONEY KWA WANAOTEMBEA NA WAUME ZA WATU

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Model na mtangazi, Gift Stanford ‘Gigy Money’amewageuka wanawake wanaotembea na waume za watu huku akionyeshwa kusikitishwa kwake na kitendo hicho na kuwashauri waache tabia hiyo.

Kupitia Ukurasa wake wa instagram, Gigyameandika waraka mrefu akiwatuhumu wanawake wa aina hiyo.

“Kama unatembea na mume wa mtu na upo huru kumpigia simu wakati wowote, anaweza hata kulala kwako na asiulizwe chochote, anaishi na wewe kama vile hana mke basi jua kuna mwanamke mwenzako anateseka na kulia kila siku. Unaweza kudhani kua huyo mwanaume ana upendo lakini ukweli nikuwa ni aina ya mwanaume ambaye ni mshenzi na mnyama kupita kiasi.

“Usidhani kwamba labda mke wake ni mjinga kwakua anavumilia, wala usije kudhani kua mke wake anamng’ang’ania huyo mwanaume. Kuna mara nyingi sana mke wake alihajaribu kuondoka lakini huyo mwanaume akamtishia, labda alishamuambia “Ukiondoka niachie wanangu, ukiondoka nakuua,

“Najua unadhani kwamba anakupenda labda ukimpindua huyo mke wake basi wewe utakua na furaha! Hapana hata akikuoa leo jua kua mwanaume kama huyo ashakua teja wa kunyanyasa, mkewe akiondoka akabaki na wewe basi jua kuwa wewe ndiyo utakua mtu wake wa kunyanyasa na atatafuta mwanamke mwingine kama wewe ili kula naye raha. Ndiyo mwanaume kama huyo anachukulia mke wake kama choo.

“Kwamba anakula raha kwengine lakini takataka zake anaenda kuweka kwa mkewe. Kwa maana hiyo akikuoa wewe basi jua ataendelea kula raha kwengine na wewe utakua ndiyo choo chake. Huna ujanja wowote, huna uzuri wowote wala hivyo viuno au mganga uloenda havijamchanganya, hiyo ni tabia yake hivyo wakati ukifurahia mwanamke mwenzako analia na kumuita mshamba usilogwe ukachukua nafasi ya mkewe kuna mwingine nawe atakuita mshamba.”

No comments:

Post a comment