Monday, 9 July 2018

DC hapi ampa agizo hili RPC

Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Mh. Ally hapi amemuagiza RPC kumkamata meneja wa dawasco na kuwekwa ndani iwapo hadi kufikia kesho saa tano na nusu ikiwa hawajashusha bomba kwenye barabara ya CCBRT, ameyasema hayo leo katika mbio za mwenge pindi kiongozi wa mbio hizo Charles Francis Kabeyo akizindua barabara hiyo.

Pia Jengo la zahanati ya mkoroshini lililopo msasani limekuwa na utata wa kutofanikiwa kuzinduliwa kutokana na ubora wa matofali hayo yanayotumika kujengea zahanati hiyo kuwa chini na kiwango ambapo yamekuwa yakimomonyoka na mengine kupasuliwa na kiongozi huyo wa mwenge.


Kiongozi wa mbio za mwenge Charles Francis amegomea rasmi kuzindua jengo la zahanati ya mkoroshini iliopo msasani kutokana na kutokidhi viwango vya ujenzi vya jengo hilo vilevile kuwa na gharama za juu kwenye ujenzi wa jengo hilo ambapo takukuru wametakwa kufatilia swala hilo kwa undani ili kuweza kubaini yaliyomo ndani ya ujenzi huo na gharama kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment