Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akishuhudia uzinduzi wa kampeni ya chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wa kuanzia miaka 9-14
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi binti kadi yake baada ya kupata chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi 
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akifurahia jambo na mabinti walioenda kupata chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi katika wilaya ya Nachingwea 
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.



MABINTI 15,521 wanatarajiwa kupata chanjo ya dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wa miaka 9-14 katika wilaya ya Nachingwea 

Akizungumza wakati uzinduzi wa kampeni Chanjo dhidi saratani ya mlango wa kizazi,mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa mabinti wa wilaya hiyo watapata chanjo wote kwa asilimia 100 ili kuokoa uhai wa mabinti hao 

Moyo alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia suluhu Hassan inatoa chanjo bure kwa mabinti wote bure kwa kulinda afya za mabinti wote wa kitanzania.

Moyo alisema kuwa chanjo zinazotolewa ni chanjo salama haina madhara yoyote kwa mabinti na serikali imekuwa inatoa chanjo salama hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dr Samia suluhu Hassan katika kuiweka jamii salama 

Kwa upande wake Mratibu wa huduma za Chanjo Wilaya ya Nachingwea Rehema  Kuchukua alisema kuwa binti asipopata chanjo anakuwa hatari kwa maisha yake 

Kuchukua alisema kuwa kampeni ya chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti itaendelea kutolewa katika hospitali 3, Vituo vya afya 5 na zahanati 44.

Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuwapeleka mabinti zao kupata chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi ili kuokoa maisha yao.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: