Friday, 18 May 2018

Tuzo za BET 2018: Afrika Mashariki hakuna msanii aliyetajwa, Nigeria na SA zaongoza

Kituo cha runinga cha BET tayari kimetangaza majina ya wasanii watakaowania Tuzo za BET 2018 kutoka Afrika katika kipengele cha Best International Act.
Katika kipengele hicho majina matano ya wasanii watakaowania tuzo hizo kutoka Afrika hakuna jina la msanii yeyote kutoka Afrika Mashariki.
Nigeria imetoa wasanii wawili Davido na Tiwa Savage, Afrika Kusini imetoa rapa Cassper Nyovest na kundi la muziki la Distruction Boyz, huku DR Congo wakiwakilishwa na Fally Ipupa.
Tuzo za mwaka huu zitafanyika tarehe 26 Mei na mshindi wa kipengele cha Best International Act atakabidhiwa tuzo kwenye jukwaa tofauti na kipindi cha nyuma.
Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa wasanii kutoka Afrika Mashariki kutemwa kwenye kwenye kipengele hicho cha Best Intenational Act. Licha ya Rayvanny mwaka jana kuinyanyua Tanzania kwa kushinda tuzo hizo kwenye kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act.
Unaweza ukampigia kura msanii wako unayempenda kupitia mitandao ya kijamii kwa kutumia hashtag ya #Ipick(jina la msanii) au unaweza kupiga kua yako HAPA.

No comments:

Post a comment