Wednesday, 30 May 2018

Serikali yaeleza imeajiri vijana wangapi katika viwanda vipya vilivyojengwa

Serikali imesema kuwa idadi ya vijana walioajiriwa katika viwanda vipya vilivyojengwa tangu serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani asilimia kubwa ni vijana.
Akizungumza leo Mei 30, 2018 akijibu kwa niaba ya Waziri wa viwanda na Biashara,Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, ajira na watu wenye ulemavu, Antony Mavunde amesema kuwa jumla ya idadi ya walioajiriwa hawezi kuipata kwa muda huo.
Akiuliza swali, Mbunge wa Viti Maalum,Khadija Ally Nasri aliyehoji, Hotuba ya viwanda na biashara ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 ilieleza kwamba tangia serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani imeshajenga viwanda 3036 je nivijana wangapi wameweza kuajiriwa mpaka sasa?
“Alitaka kujua idadi ya vijana walioajiliwa katika viwanda kwasababu idadi hii ya walioajiri katika viwanda siwezi kuipata hapa ndani bungeni hivi sasa ntakachokifanya nikuhakikisha tunafanya coordination ya kutaka kujua katika viwanda vilivyotoa ajira kwa vijana ni asilimia ngapi ya vijana wamekwisha kupata ajira mpaka hivi sasa, lakini niseme kwamba kutokana na mchango miwngi kutoka sekta ya viwanda tunaamini ni kundi kubwa la vijana ndio walioajiriwa kwasababu katika nguvu kazi yetu ya nchi tulionayo asilimia zaidi ya 65 ni vijana kwahiyo automatically asilimia kubwa waliopata ajira ni vijana,” amesema Mavunde.

No comments:

Post a comment