Sunday, 27 May 2018

Serikali imezindua kituo cha kisasa cha kupima Ebola


 
Katika kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Ebola leo May 27, 2018 nakusogezea stori kuhusu Serikali imefungua kituo cha kisasa cha kupima na kugundua virusi vya Ebola katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akikagua kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile ameagiza maafisa wa uhamiaji kuhakikisha kwamba wasafiri wote wanaotumia uwanja huo wanapimwa. Aliongeza kuwa serikali pia imefungua kwenye uwanja huo zahanati maalum ya kutibu wasafiri watakaopatikana na Ebola.

“Tunajitahidi kuhakikisha kwamba ugonjwa huo hauingii nchini,” alisema Ndugulile.  Ugonjwa wa Ebola uligunduliwa katika nchi jirani ya DRC ambapo tayari imeua watu 20.

No comments:

Post a Comment