Friday, 13 April 2018

TTCL Kuanza kukata tiketi za Udart Kampuni ya Usafirisha wa mabasi yaendayo Haraka(Udart), imemaliza mkataba na Max Malipo Africa katika ukataji wa tiketi na sasa huduma hiyo itafanywa na Kampuni ya Simu(TTCL).

Hayo yamesemwa leo Aprili 13, na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa kampuni hiyo, Deus Bugaywa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadiliko hayo.

Amesema mabadiliko hayo ni moja ya njia ya kuboresha huduma zao ambapo TTCL kutokana na kuwa na mkongo wa taifa wanaamini wateja wao watapata huduma iliyo bora.

Kuhusu wafanyakazi waliokuwa wakikatisha tiketi, amesema wataendelea na ajira zao kwani hata awali walikuwa wanaripoti kwa Max Malipo lakini masuala ya mshahara walikuwa wakipewa na Udart.

"Katika mabadiliko hayo sasa wakata tiketi hawa wataripoti TTCL na mshahara kuendelea kupewa na Udart,"amesema Bugaywa.

No comments:

Post a comment