Thursday, 12 April 2018

Tetesi: Kocha wa Singida United Mholanzi, Hans van der Pluijm kutimkia Azam FC

Kocha Mkuu wa klabu ya Singida United Mholanzi, Hans van der Pluijm huwenda akaingia mkataba na matajiri wa jiji la Dar es salaam timu ya Azam FC kufuatia timu hiyo kushindwa kufanya vema kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara kwa misimu miwili sasa.
Taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa Azam FC ambayo inashika nafasi ya tatu kwa kujikusanyia pointi 45 inaweza kuachana na Kocha wake raia wa Romania, Aristica Cioaba na mikoba yake kurithiwa na Pluijm ambaye amekuwa na rekodi nzuri zaidi kwenye mashindano mbalimbali ya hapa nyumbani.
Kabla ya kutua Singida United kocha, Hansa Van Pluijm alitokea Yanga SC ambapo alijiunga msimu wa 2013-14 na kuifikisha timu hiyo nafasi ya pili ligi kuu Tanzania Bara nyuma ya Azam FC walionyakua ubingwa huo kwa mara ya kwanza.
Msimu wake wa mafanikio ndani ya Yanga SC ukiwa ni mwaka 2015-16 baada ya kurudi tena kupokea timu kwa mbrazili Macio Maximo. Msimu wa ligi kuu 2015-16 Hans Van Pluijm aliiwezesha timu hiyo kutwaa kombe la ligi kuu ikiwa imecheza michezo 30 na kupoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Coastal Union mjini Tanga na kwenda sare mechi 7.
Rekodi ya kupoteza mechi 1 tu katika mechi 30 huku mchezaji wake, Amisi Tambwe akiibuka mfungaji bora wa ligi kuu kwa goli 21 hii inaonesha uwezo wa kocha huyo wa kuisuka vema timu yake katika safu ya ulinzi na ushambuliaji.
Msimu huo huo wa 2016, Pluijm aliiwezesha Yanga kutwaa kombe la FA baada ya kushinda mechi zote saba toka mechi za mtoana, robo fainali, nusu fainali na fainali dhidi ya Azam FC.
Hii ni jumla ya mechi 29 kati ya mechi 37 katika kombe la ligi kuu na na FA Pluijm aliiwezsha Yanga kushinda kwa msimu wa 2015-16.
Hatua ya awali kombe la klabu bingwa barani Afrika Pluijm aliiwezsha Yanga SC kushinda mechi 3. Alishinda dhidi ya Cercle de Joachim nyumbani na ugenini ikiwa ni jumla ya mechi 2 pia akishinda mechi moja dhidi ya APR na kutoka sare mechi ya marudiano jijini Dar.
Hatua ya pili klabu bingwa alikwenda sare mara moja dhidi ya Al Ahly jijini Dar ( 1-1 ) na kufungwa 2-1 jijini Alexandria Misri. Hii ni wastani wa kushinda mechi 3 klabu bingwa , sare 2 na kufungwa mechi 1.
Kombe la Shirikisho Hans Van Pluim alishinda mechi 2 tu moja ikiwa hatua ya raundi ya pili dhidi ya Esperanca Sagrada 2-0 jijini Dar na kufungwa 1-0 nchini Angola. Hatua ya nane bora alishinda mechi 1 tu dhidi ya MO Bejaia jijini Dar na kupoteza mechi 5.
Msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara mechi ya Ngao ya Jamii alipoteza kwa matuta dhidi ya Azam FC lakini ameweza kuiongoza Yanga SC kushinda mechi 6 sare 3 na kufungwa mechi 1 pekee kwa kushika nafasi ya 2 katika ligi na alama 21.
REKODI MUHIMU
Anashikiria rekodi ya kocha bora wa msimu wa 2015-16
REKODI KITIMU
– Mabingwa ligi kuu msimu wa 2015-16
-Mabingwa kombe la FA msimu wa 2015-16
– Kufika raundi ya pili klabu bingwa Afrika 2016
– Kufika hatua ya nane bora kombe la shirikisho2016

No comments:

Post a comment