Friday, 13 April 2018

TANESCO yaeleza sababu ya kukatika kwa umeme


Shirika la Umeme nchini, TANESCO limetangaza kutokana na kukosekana umeme katika maeneo mengi nchini ni kutokana na hitilafu iliyosababishwa na Radi kupiga  mifumo ya usambazaji wa umeme katika gridi ya taifa.
“Kutokana na tatizo la umeme limejitokeza TANESCO tumefanya juhudi kurejesha hali ile, tulianza kurejesha Tanga, Chalinze kupitia kituo cha New Pangan, Dodoma kupitia kituo cha Mtera na sehemu ya kituo cha kidatu” amesema  Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dkt. Titus Mwinuka.

No comments:

Post a comment