Wednesday, 11 April 2018

Serikali yakubaliana na Bulaya, yampa ahadi


Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekubalina  na hoja iliyotolewa na Mbunge Ester Bulaya kuwepo kwa changamoto la upungufu wa walimu wa sayansi katika jimbo lake na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa madai ni tatizo la nchi nzima sio kwake pekee.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ole Nasha leo Aprili 11, 2018 kwenye kikao cha saba mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo linafanyika Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la nyongeza la Bulaya aliyetaka kujua ni lini serikali itaamua kupeleka walimu wa sayansi katika jimbo lake kwa kuwa amechoshwa na wilaya yake kuwa miongoni inayofanya vibaya katika masomo hayo.

"Ni kweli upo uhaba wa walimu wa sayansi nchi nzima. Naomba nimuhakikishe Bulaya kuwa tunafahamu uwepo wa upungufu nasio katika Jimbo la Bunda pekee, kwa hiyo tutaendelea kuhakikisha kwamba upungufu huo tunaufanyia kazi ipasavyo", amesema Ole.

Kwa upande mwingine, Ester Bulaya amesema halmashauri yake imepata walimu ambao hawazidi hata 60 katika masomo yote na kuanza kufafanua kama ifuatavyo, walimu wa hisabati mahitaji ni 55 waliopo 20 pekee yake, fizikia mahitaji 27 waliopo 10, Biologia mahitaji 32 waliopo 15, huku akidai Chemistri kidogo ndio wamejitahidi kutoa walimu wengi kwa kuwa mahitaji 29 waliopo 21 bado 8

No comments:

Post a comment