Tuesday, 24 April 2018

Mazoezi ya Polisi Kilimanjaro yazua taharuki

Leo April 24, 2018 majira ya asubuhi Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limefanya mazoezi kwa vitendo baadhi ya maeno katika mji wa Moshi kitu kilichozua taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.

Taarifa kutoka Moshi zinaeleza kuwa shughuli katika mji huo leo zimesimama kwa muda kufuatia zoezi hilo ambalo polisi walikuwa na silaha za moto.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hamis Issah amesema zoezi hilo ni la kawaida kwa askari Polisi na kwamba wamekuwa wakipata mafunzo ya nadharia kwa muda mrefu sasa wameamua kuyafanya kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment