Afisa Habari wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC, Haji Manara amefunguka na kudai kipigo walichokipata Yanga jana Aprili 29, 2018 cha bao 1-0 ni cha heshima kutokana na wao kuwa mabingwa watetezi hivyo isingekuwa vizuri kuwadharaulisha mbele ya umati wa mashabiki.

Manara ametoa kauli hiyo mara baada ya 'Kariakoo Derby' kumalizika katika uwanja vya Taifa Jijini Dar es Salaam huku timu yake ikiwa imetoka na ushindi wa bao 1 lililofungwa mnamo mwa dakika 38 kupitia Erasto Nyoni kwa kutumia kichwa akiunganisha krosi ya Kichuya.

"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumepata matokeo ila hatujaridhika bado mpaka tuwe mabingwa, 'perfomance' yetu kwa ujumla ilikuwa nzuri ndio maana hata 'corner' moja wenzetu hawakuweza kupata lakini sisi vilevile tulicheza kwa heshima", amesema Manara.

Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "kipindi cha kwanza kilipomalizika nilishuka chini nikazungumza na wachezaji wangu kuwa waende wakawafunge Yanga kwa heshima kwasababu wao ni mabingwa watetezi na msiende kuwafunga kwa dharau kwa hiyo niliwapa maelekezo madhuri vinginevyo tungewadharaulisha kwa kuwafunga mabao 5, 6 kwa hiyo tumewafunga kwa heshima kutokana ni wakubwa wenzetu".

Kutoka na ushindi walioupata jana Simba sasa wamekuwa wamefikisha alama 62 kwenye mechi 26 huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi kuu msimu huu. Simba inabakiza alama 4 pekee ili iweze kuwa bingwa msimu huu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: