Friday, 13 April 2018

Mabosi wa Yanga wakutana Usiku kumjadili Lwandamina


George Lwandamina.

KAMATI ya Utendaji ya Yanga, juzi usiku ilikutana haraka kujadili suala kuondoka kwa kocha wao Mzambia, George Lwandamina aliyejiunga na Klabu ya Zesco United ya nchini huko.

Taarifa zilizotolewa jana na Zesco ni kwamba wamemalizana na kocha huyo ambaye anachukua mikoba ya kocha wa muda, Tenant Chembo aliyejiuzulu Jumapili iliyopita.

Kocha huyo aliondoka juzi Jumanne na kurudi nyumbani kwao kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa kukinoa kikosi hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema wajumbe wa kamati ya utendaji wote walikutana juzi baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

“Ni mapema kuanza kulizungumzia suala la Lwandamina kwa sasa kwa sababu jana (juzi) kamati ya utendaji ilikutana kujadili ili kulipatia ufumbuzi suala hilo. “Hivyo, katika kikao hicho baadhi ya mambo tumejadili na kufi kia muafaka mzuri, hivyo ningepewa muda kidogo na baada ya kufi kia muafaka mzuri tutalitolea ufafanuzi,” alisema Nyika.

Aidha, imeelezwa kuwa kamati hiyo imekubaliana kumpitisha kocha wa viungo Noel Mwandila kusaidiana na Shadrack Nsajigwa katika kipindi hiki cha mpito.

No comments:

Post a comment