Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amefunguka kuwa mpaka sasa haelewi ni kwa vipi mtu anaweza kuuwawa na polisi kwa kuchomwa kisu tena akiwa amefungwa pingu huku akikumbushia tukio la mdogo wake mwingine kujeruhiwa vibaya na polisi ambapo alisababishiwa ulemavu mwaka jana.

Mbunge Heche amesema kwamba mtu kuchomwa kisu mgongoni ni kudhamiria kuua kwasababu mtu huyo hakuwa anapambana.

"Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi mtu anaweza kuuawa na polisi kwa kuchomwa kisu tena akiwa amefungwa. Kuchoma mtu kisu mgongoni ni kudhamiria kuua kwasababu hakua hata anapambana.Nilijua mikononi mwa polisi ni sehemu salama.

"Wiki mbili zilizopita kijana Allen alikufa katika maizingira tata kule Mbeya.

"Leo ni kwangu mdogo wangu ameuwawa kikatili sana mikononi mwa polisi.Maisha yangu yote nimeyatoa kupigania haki ili watu wasionewe, mtuhumiwa  asifanywe mkosaji na kuhukumiwa kabla ya vyombo vya sheria kumhukumu.

"Mwaka jana mdogo wangu mwingine aliumizwa vibaya sana na polisi. IGP Mangu na RPC aliyekua Tarime walilipa uzito suala hilo lakini alipoondolewa, suala liligeuzwa kisiasa na wale vijana waliokua wamemjeruhi mdogo wangu ambae mapaka sasa sikio moja halisikii, wakarudishwa kazini kinyemera na kuhamishwa Tarime kama kunikomoa.

"Mimi nimewahi kutishiwa kuuawa kituo cha polisi, najisikia maumivu makubwa mno lazima Watanzania wakatae hali hii. Waziri yuko kimya, wangapi wanakufa na kuumizwa mikononi mwa polisi bila matukio kujulikana wala kutangazwa? Nitazungumza mda ukifika." Amesema John Heche,
Share To:

msumbanews

Post A Comment: