Friday, 13 April 2018

ABB YAZINDUA HUDUMA YA DHARULA YA SEKUNDE 15


Mitambo ya huduma ya dharula (Emergency Lighting) ndani ya jumba la Sandton Convention Centre, Johannesburg, Afrika Kusini.
Vibao tofauti vya huduma ya dharula (Emergency Lighting).
Baadhi ya wahudhuriaji katika onesho hilo.
Wahudhuriaji wakielekezwa baadhi ya vifaa vinavyotumika katika viwanda vya vyakula na vinywaji.
Muundo wa makao makuu ya ABB, Zurich, Uswisi.
Baadhi ya vifaa vinavyofungwa katika mashine za vyakula na kutengeneza vinywaji.
Mkuu wa Kitengo cha Utengenezaji wa Roboti katika Viwanda kutoka ABB, Sami Atiya akiongea na wahudhuriaji katika onesho hilo (hawapo pichani).
Mkuu Kitengo cha Uzalishaji wa Umeme wa Sola, Haluk Ozgan akimuelekeza mhudhuriaji juu ya utumiaji wa umeme wa sola.
Wahudhuriaji wakielekezwa kuhusu utengenezaji na ufungaji wa transfoma.
KAMPUNI ya ASEA Brown Boveri (ABB) inayohusika na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vikubwa vya umeme duniani, imezindua huduma ya dharula (Ermegency Lighting) inayotumia sekunde 15.

Akiizungumzia huduma hiyo wiki hii ndani ya Jengo la Sandton Convention Centre, Johannesburg nchini Afrika Kusini, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Claudeen Forbes alisema, ABB inatambua umuhimu wa kila mmoja katika jamii hasa linapotokea tatizo hivyo huduma hiyo ya dharula itasaidia kwa kiasi kikubwa majengo ya ofisi, hoteli, shule, hospitali, uwanja wa ndege na treni pale kunapotokea janga la moto ambapo hutumia saa 24 kwa siku 7.

“Huduma hii ya dharula (Emergency Lighting) kwanza inafanya jengo kuwa na usalama pili ni ya kupapasa wakati wa kuitumia (touch screen) na pia ni rahisi kuiseti na kuanza kuitumia.

“Huduma hii inamuwezesha mtu anayeishi kwenye jengo iwe hospitali, ofisi, shuleni au popote pale linapotokea tatizo la moto kuweza kuiwasha ambapo hutumia sekunde 15 tu milango kujifungua na hukaa zaidi ya saa tatu,” alisema Claudeen.

Mbali na hiyo, Jumanne na Alhamisi kulikuwa na onesho kubwa la ABB ndani ya ukumbi huo ambapo vitu mbalimbali walivizindua kama vile gari linalotumia umeme wa DC, transfomer, mashine mbalimbali zinaztotumika katika viwanda vya vyakula na vinywaji, teknolojia ya utumiaji wa roboti (Yumi) katika viwanda, jinsi ya kuthibiti utapeli wa mitandaoni, umeme wa sola pamoja na huduma ya kisasa ya mtandao ya 5G jinsi inavyokuja kuiteka dunia.
PICHA, STORI: Andrew Carlos aliyekuwa Afrika Kusini.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: