Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Julieth Magandi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla kukabidhiwa vitanda 14 na magodoro 12 ambayo yametolewa na Australia Tanzania Society. Kulia ni Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
 Muuguzi Alice Msonda na Velena Joahackim wakitandika kitanda baada ya kukabidhiwa vitanda na magodoro na Australia Tanzania Society.
 Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi vitanda 14 leo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akizungumza na waandishi wa habari leo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vitanda 14, magodoro 12  pamoja na drip stands kutoka Australia Tanzania Society ambavyo vitasaida kuimarisha utoaji wa huduma hospitalini  hapo.

Akipokea msada huo jijini Dar es Salaam  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt.  Juliethi Magandi amesema kwa muda mrefu hospitali imekua na ushirikiano na tasisi hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo kufanya  upasuaji wa ubingwa wa juu.

“Kipekee nichukue fursa hii kuwashukuru rafiki zetu hawa Australia Tanzania Society kwa msaada huu  walioutoa kwani tumekua tukishirikiana kwa zaidi ya miaka mitatu sasa,”.  amesema Dkt. Magandi.

Amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina jumla ya vitanda 1,507 na kwamba kina mama wajawazito na watoto pekee wanatumia karibu  ya nusu ya vitanda hivyo.  “Hivyo  msaada huo umekuja wakati muafaka  kwani hospitali bado ina mahitaji kutokana na kutoa huduma zake kila siku kwa saa 24,”.

 “Kati ya vitanda hivi 14 tulivyopewa leo, sita tumevileta wodi 35  kwa ajili ya kina mama na vingine 8 tumepeleka ICU namba moja na ICU namba mbili’’ amefafanua Dkt. Magandi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo amesema msaada huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 25 na kwamba lengo ni kuboresha huduma za afya hususani katika hospitali za Umma.

“Kutoa ni moyo si utajiri tutaendelea kushirikiana katika kuboresha huduma za afya kadiri hali inavyoruhusu  nitoe wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana ili tuboreshe huduma za afya nchini ‘’amesema Bwana Chialo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: