Marekani imesikitishwa  na taarifa za kutekwa na utumiaji nguvu kikatili uliosababisha kifo cha Katibu wa Chadema kata ya Hananasif Daniel John.
Taarifa kutoka ubalozi wa Marekani kwa vyombo vya Habari Leo Februari 15 imesema  kwamba  mauaji hayo yanaongeza uhasama.
‘’Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu kwa msiba huu’’ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilisema tukio hilo la mauji la makabiliano ya kihasama na vitendo vya kikatili ni jambo linalotia wasiwasi na kusikitisha sana.
‘’Tunatoa wito kwa vyama vyote kulinda amani na usalama wa mchakato wa kidemokrasia, taifa na wa watu wa Tanzania’’ilisema taarifa hiyo na kuongeza  
 ‘’Tunaungana na Watanzania katika kutoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wenye uwazi ili kuwawajibisha wale wote wanaohusika na vitendo hivi vya kikatili kwa mujibu wa sheria za Tanzania’’

Share To:

msumbanews

Post A Comment: