Monday, 12 February 2018

Lowassa amuomba Rais MagufuliWaziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Mhe. Edward Lowassa amefunguka na kuiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kusikiliza maoni ya wananchi wanayotoa katika mambo mbalimbali na kuyachukulia hatua stahikiLowassa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akimuombea ridhaa mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu ili aweze kupata kura za ndio kwa wananchi hao siku ya kupiga kura ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo, huku akisindikizwa na mameya na Wabunge mbalimbali kutoka UKAWA.

"Ningependa kuchukua nafasi hii kuiomba serikali isikilize maoni ya wananchi. Serikali yeyote duniani huongozwa na 'public opinion', kwamba wanasema nini wananchi, haiwezekani wananchi wakawa wanasema halafu hakuna hatua yeyote kwa serikali. Tunaiomba isikilize maoni ya wananchi", amesema Lowassa.

Kwa upande mwingine, Edward Lowassa amelishukuru Baraza la Maaskofu Tanzania kwa kuweza kuwaunga mkono upinzani na wapenda mabadiliko katika kutetea haki za wanyonge katika nchi.

No comments:

Post a comment