Imeelezwa kuwa matumizi ya Nishati safi ya kupikia sio anasa bali ni muhimu kwa kutunza mazingira na afya za wananchi,na pia inasaidia kupunguza muda wa uzalishaji  ambapo kwa sasa wananchi wanatakiwa kuhama katika tamaduni za kubaki kutumia nishati isiyo safi na kutumia nishati safi ya kupikia.

hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba alipokutana na Bodi ya Wakala wa Nishati Vijini (REA),katika Ofisi za REA zilizopo jijini Dodoma,Novemba 25, 2025 ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake kwenye taasisi zilizoko chini ya Nishati.

"Natoa rai kwa watanzania kuwa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia sio anasa bali kwanza yanasaidia kutunza mazingira , pili yanasaidia kupunguza muda wa uzalishaji ambao mwanamke anakaa jikoni muda mrefu kupika wakati ukitumia nishati safi na inaokoa zaidi ya asilimia 70% ya muda ambao unatumia kupika".

Aidha, amesisitiza kwa wananchi wote kubadilika na kwenda na wakati sambamba na kwenda na kasi ya Dunia inavyoenda,ambapo kwa sasa matumizi ya kuni na matumizi ya Mkaa  kwa sehemu kubwa ya dunia hawatumii kabisa,  hivyo tunatakiwa kwenda kwa kasi hiyo ili watu wote  watumie nishati safi ya kupikia.

Nishati safi ya kupikia ni kapaumbele cha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, hivyo kama serikali inaendelea kutoa ruzuku ili kuhakikisha wananchi wanapoenda kujaza au kunua mitungi gesi  bei inakua pungufu,  pia Serikali inaweka juhudi kubwa kuhakikisha vituo vya ujazaji wa gesi katika mitungi inakua karibu na  wananchi walipo.

Aidha, Mhe. Makamba ameongeza kuwa mipango mingi ambayo Serikali imejiwekea ipo ile mingi ambayo ni ya muda mfupi na michache ya muda mrefu,  lengo likiwa ni kuendelea kutekeleza ahadi ya Mhe. Rais ya  kuwafikishia wananchi umeme kwenye vitongoji.

Ameongeza kuwa Wizara ya Nishati kupitia  REA inaendelea kutekeleza mpango wa kuvifikia vitongoji 9000 kwa kipindi hiki kifupi na kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika.

Sambamba na hilo Mh. Rais amekua kinara wa Nishati safi ya kupikia na amezungumzia sana juu ya suala hili katika majukwaa mbalimbali , hivyo basi kwa upande wa nishati safi ya kupikia Wizara kupitia REA ndani ya muda huu mfupi imeandaa mradi wa muhsusi kuhakikisha taasisi zaidi ya hamsini (50) zinapata nishati safi ya kupikia na hizi ni taasisi ambazo zina idadi ya watu kuanzia 100 na zadi, ili kuweza kupunguza uharibifu wa mazingira pamoja na kuokoa muda ambao taasisi zinatumia kwa ajili ya kutengeneza chakula.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya wakala wa nishati vijijini- REA Mha.Hassan Said amesema kuwa mpango wa serikali  ni kuhakikisha kasi ya kuwaunganishia umeme wananchi katika vitongoji unakua endelevu na kuongeza kuwa hali ya upatikanaji wa umeme inaongezeka.

Amesema jumla ya vitongoji vilivyopo nchini ni  64,359 kati ya hivyo vitongoji 39,000 tayari vimepatiwa umeme ikiwa ni sawa na  asilimia 60%  vilivobakia ni vitongoji 25,400 kati ya hivyo vitongoji 2,500 miradi inaendelea wakati vitongoji 9,000 Wakala upo katika hatua ya mwisho ya utiaji saini ili vifikishiwe umeme.

Aidha Mhe. Naibu waziri alifanya ziara ya kufanya ziara kutembelea Kituo cha kupoza na kusafirisha umeme cha Zuzu kwenda kujionea hali ya kituo,kazi inayofanyika sambamba na hatua za ujenzi iliyofikiwa kwa baadhi ya maeneo ya kituo hicho zinavyoendelea.













Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: