Halmashauri ya Jiji la Arusha imeanza mchakato wa kuwasilishi mapendekezo ya bajeti  mpya ya mwaka 2018/19 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 6.9 zitatengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kuwaudumia wananchi hususan katika sekta ya afya,elimu na miundombinu ya barabara.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Athumani Kihamia amesema kuwa tayari wameanza kukaa vikao vya mapendekezo ya bajeti na Watendaji wa Kata,Viongozi wa Dini,Makundi ya Wazee na Vijana ili kupata maoni yao juu ya vipaumbele vya bajeti hiyo ili iweze kutatua changamoto ya wananchi iwapo itatekelezwa kama ilivyopangwa.

Kihamia aliyasema hayo wakati akizungumza katika kikao cha mapendekezo ya bajeti kilichofanyika katika ukumbi ulioko katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha,ambacho kilihudhuriwa na wadau mbalimbali.

Baadhi ya wajumbe wamependekeza kuwekwa kipaumbele katika suala la ujenzi wa madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani jambo ambalo litasaidia kuboresha maendeleo ya taaluma mashuleni.

Kufuatia Ongezeko la Ufaulu wa Wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza ,MKuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuhakikisha wanajenga madarasa ya kutosha ili kuepusha msongamano na uhaba wa vyumba vya madarasa katika kipindi cha mwanzoni mwa mwaka ambacho wanafunzi wengi hujiunga na masomo ya sekondari.

Akizungumza katika kikao cha Mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2018/19 ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata 25 zilizoko jiji la Arusha ,Daqqaro amesema kuwa watendaji wa serikali wanapaswa kuachana na tabia ya kuwajibika pindi wanapoona wanafunzi wamekosa madarasa na badala yake watenge fedha za kujenga madarasa mapema .

Naibu Meya wa Jiji la Arusha Viola Lazaro alisema kuwa hulka ya baadhi ya watendaji  kushughulikia tatizo la uhaba wa madarasa kipindi ambacho kina idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari  imekua ikiwagharimu watoto kushindwa kufanya vizuri kitaaluma kutokana na msongamano wa wanafunzi 



Tito Cholobi Afisa Tarafa Elerai  alisema kuwa ni vyema serikali ikatenga fedha kwa ajili ya kujenga madarasa ya kutosha angalau madarasa 160 kwa kila mwaka ili kuziba pengo la uhaba wa madarasa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Athumani Kihamia amesema kuwa serikali itajitaidi kuhakikisha kuwa inajenga madarasa ya kutosha kwani ni kipaumbele cha serikali kuboresha elimu na taaluma kwa ujumla.










Share To:

msumbanews

Post A Comment: