Articles by "WANAWAKE"
Showing posts with label WANAWAKE. Show all posts

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.

Na Gideon Gregory, Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewahimiza wakina mama wa kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanajifunza kwa makini na kuwa tayari kupokea mafunzo watakayopatiwa na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) kwani yatawasaida kwenda kuajiliwa na kuwa watumishi bora.

Senyamule ameyasema hayo leo Machi 24,2025 Jijini Dodoma wakati akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya wanawake hao na kuongeza kuwa watakuwa watumishi bora kwasababu wametoka kwenye mafunzo ya VETA yenye ujuzi na utaalamu wa ufundi wanaoufanyia kazi.

"Mimi nina imani kuwa mafunzo haya yatakwenda kuleta mapinduzi katika sekta ya huduma hizo mnazojiajili ndani ya mkoa wa Dodoma, hivyo nitoe pongezi kwa Mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Dodoma kwani anafanya kazi nzuri sana na ndiye amefanikisha hili kwa juhudi zake anazozifanya,"amesema.

Aidha amesema kuwa wanawake wengi hawana ujuzi ndiyo maana hata kujiajili ili watoe huduma mbalimbali imekuwa changamoto pia hawana mitaji jambo linalopelekea wakipewa tenda za kazi kutatamani kukimbia.

"Unaweza ukampa tenda akasema napata wapi mtaji wa kutoa hiyo tenda, lakini bado kuna suala la nidhamu ya kazi yeye anajua pia akipata kazi anaifanyaje,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore amesema katika mafunzo wanayoyatoa eneo waliloliwekea mkazo ni kuhakikisha wanawake wanaodahiliwa katika vyuo vya ufundi stadi wanaongezeka hadi kufikia 45% .

"Sasa hivi tunapata changamoto tuko 27% kunamuda tunakuwa hapo tunafika 35% lakini lengo letu tunataka tufike 45% wawe ni wanawake na kuweza kufikia haya tunayo mafunzo mbalimbali ambayo tunahitaji tuweze kuyafanya ili kuhakikisha sasa eneo hili la kufikia asilimia hizo tunazifikia,"amesema.

Awali Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma Deodatus Orotha amesema dhumuni la kuandaa mafunzo hayo ni kuwapatia ujuzi wanawake wa Mkoa wa Dodoma ili waweze kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii yao pamoja na familia zao na hivyo kuleta tija kwa taifa.

"Lengo ni kuwafikia wanawake wa Mkoa wa Dodoma wapatao 3000 na hivyo utaratibu utakuwa kwa hawamu na kwa kuanza tutaanza na wanawake 250 watakapomaliza watakuja wengine 250 mpaka tuweze kufikia idadi yetu ya mwisho tuliyoilenga,"amesema.

Naye Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Bi. Fatuma Madidi amesema wamefurahia fursa hiyo na wako tayari kujifunza hivyo wanaamini kupitia mafunzo hayo wataenda kuwa bora, wajuzi na kuongeza kipato na hali ya wanwake kuonekana ombaomba inakwenda kuondoka.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.

Mkuu ww Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA. Anthony Kasore akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma Deodatus Orotha akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.

Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Bi. Fatuma Madidi akizumgumza kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.

Wanawake wa kikundi cha wanawake na Samia mkoa wa Dodoma kwenye ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi chao.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akifungua kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.

Picha ya pamoja ya washiriki wa ufunguzi wa kozi mbalimbali za muda mfupi kwaajili ya kikundi cha wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma.

 

Wanafunzi na Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto wanaotoka kwenye mazingira hatarishi wakiwa katika eneo la bustani kwa ajili ya kupata elimu juu ya kilimo cha Mboga kutoka kwa Wanawake watafiti kutoka taasisi ya kimataifa ya utafiti wa Mboga Duniani "World Vegetable Center ya jijini Arusha ambao waliwatembelea watoto hao .
Mtafiti  Bi. Inviolate Mosha kutoka taasisi ya kimataifa ya utafiti wa Mboga Dunia "World Vegetable Center",akiwafundisha watoto katika kituo cha kulea watoto cha Motonyoki kilichopo Olasiti jijini Arusha namna ya kuotesha mboga .
Mtafiti  Bi. Inviolate Mosha kutoka taasisi ya kimataifa ya utafiti wa Mboga Dunia "World Vegetable Center",akiwafundisha watoto katika kituo cha kulea watoto cha Motonyoki kilichopo Olasiti jijini Arusha namna ya kuotesha mboga ,zoezi hilo likishuhudiwa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Colleta Ndungulu (wa pili kutoka kulia) walioshika majembe.
Sehemu ya timu kutoka taasisi ya kimataifa ya utafiti wa Mboga Dunia "World Vegetable Center",wakishuhudia namna ambavyo watoto katika kituo cha kulea watoto wanaotoka kwenye mazingira hatarishi cha Motonyok kilichopo Olasiti jijini Arusha wakifundishwa juu ya uoteshaji wa mboga 
Mtafiti Leticia akiwa akirejesha tabasamu kwa mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Motonyok walipofika kutoa elimu .
Sehemu ya timu kutoka taasisi ya kimataifa ya utafiti wa Mboga Dunia "World Vegetable Center",wakishuhudia namna ambavyo watoto katika kituo cha kulea watoto wanaotoka kwenye mazingira hatarishi cha Motonyok kilichopo Olasiti jijini Arusha wakifundishwa juu ya uoteshaji wa mboga .
Sehemu ya timu kutoka taasisi ya kimataifa ya utafiti wa Mboga Dunia "World Vegetable Center",wakiongozwa na Mkurugenzi wake Colleta Ndungulu wakijadiliana jambo wakati wa utoaji elimu kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto wanaotoka kwenye mazingira hatarishi cha Motonyok kilichopo Olasiti jijini Arusha.
Mtafiti  Bi. Inviolate Mosha kutoka taasisi ya kimataifa ya utafiti wa Mboga Dunia "World Vegetable Center",akiwafundisha watoto katika kituo cha kulea watoto cha Motonyoki kilichopo Olasiti jijini Arusha namna ya kukinga mbegu baada ya kuzisia kwenye udongo .
Baadhi ya watoto katika kituo cha kulea watoto cha Motonyok kilichopo Olasiti jijini Arusha wakisoma vipeperushi vikionesha namna ambavyo kilimo cha Mboga kinafanyika .
Mtafiti Dkt Judith Hurbert kutoka taasisi ya kimataifa ya utafiti wa Mboga Dunia "World Vegetable Center",akiwafundisha watoto katika kituo cha kulea watoto cha Motonyoki kilichopo Olasiti jijini Arusha namna ya kukinga mbegu baada ya kuzisia kwenye udongo .
Mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa Mboga "World Vegetable Center" Colleta Ndunguku akiotesha mti wa kumbukumbu katika kituo cha kituo cha kulea watoto cha Motonyok kilichopo Olasiti jijini Arusha 

Na Dixon Hussein .

Arusha – Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa vitendo, wanawake wa Taasisi ya Utafiti wa Mboga Duniani (World Vegetable Center) waliamua kupeleka elimu ya kilimo cha mboga kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Matonyok kilichopo kata ya Olasiti, jijini Arusha.

Badala ya sherehe za kawaida, wanawake hawa waliamua kutumia siku hiyo muhimu kuwapatia watoto ujuzi wa uandaaji wa shamba na uoteshaji wa mboga, ili kuwasaidia kupata lishe bora na kuboresha afya zao. Mbali na elimu hiyo, walitoa msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo mchele, sukari, sabuni, na nguo, hatua iliyowafanya watoto hao kujihisi kupendwa na kuthaminiwa.

Mkurugenzi wa kituo cha Matonyok, Bi. Emmy Nicholaus Sitayo, alieleza kuwa kituo hicho kilianzishwa mwaka 2006 kwa lengo la kuwahifadhi na kuwalea watoto wanaoishi katika mazingira magumu, wakiwemo wale waliokumbwa na vitendo vya unyanyasaji kama vile ukatili wa kijinsia, kupigwa, na kunyimwa haki zao za msingi. Hadi sasa, kituo hicho kinahudumia watoto 58, kati yao 30 wakiwa wasichana na 28 wavulana.

“Tunashukuru ujio wa wanawake wa World Vegetable Center, si tu kwa msaada walioleta, bali kwa elimu ya kilimo cha mboga walichowapa watoto wetu. Kupitia maarifa haya, watoto wataweza kupata mboga kwa chakula chao cha kila siku na hatimaye kuwa na lishe bora inayosaidia kuimarisha kinga zao za mwili,” alisema Bi. Sitayo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa World Vegetable Center, Bi. Colleta Ndungulu, alisema kuwa wanawake wa taasisi hiyo waliguswa na hali ya watoto wa Matonyok na waliamua kushiriki kwa vitendo katika kuwapa ujuzi wa kujitegemea badala ya msaada wa muda mfupi.

“Tumeona ni muhimu kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapa ujuzi wa kilimo cha mboga ili waweze kujitegemea na kupata lishe bora. Hii ni sehemu ya juhudi zetu za kuhakikisha kuwa jamii ina uelewa wa umuhimu wa mboga katika afya na lishe,” alisema Bi. Colleta.

Mbali na uandaaji wa shamba na upandaji wa mboga, watoto hao pia walifundishwa kuhusu makundi mbalimbali ya vyakula na umuhimu wa kula lishe kamili. Mtafiti wa World Vegetable Center, Bi. Inviolate Mosha na Dkt Judith Hurebert , aliwahimiza watoto hao kula mlo unaojumuisha vyakula vya aina zote, ikiwemo nafaka, mizizi, nyama, samaki, maharage, na matunda, ili kujenga miili yenye afya.

Watoto wa Matonyok walionyesha shukrani kwa fursa hiyo, wakisema kuwa elimu waliyopewa itawasaidia si tu katika kituo chao, bali pia katika maisha yao ya baadaye. “Sasa tunajua jinsi ya kupanda mboga na kuzitunza hadi kuvuna. Tutakuwa na chakula chetu wenyewe,” alisema mmoja wa watoto kwa furaha.

Hatua hii ya wanawake wa World Vegetable Center ni mfano wa jinsi taasisi na makundi mbalimbali yanaweza kushiriki kikamilifu katika kubadili maisha ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Kwa kutumia Siku ya Wanawake Duniani kwa vitendo, wameleta mwanga mpya kwa watoto wa Matonyok, wakiwa na matumaini ya maisha yenye afya bora na ustawi endelevu.



Wanawake nchini wamehimizwa kuendelea kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya madini ikiwemo kuwekeza kwenye shughuli za uchimbaji pamoja na kutoa huduma migodini kwa kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa kila mtu kushiriki katika uchumi wa madini bila kujali jinsi yake kwa kuzingatia Sheria na taratibu zinazotakiwa kufuatwa.

Wito huo ulitolewa Mjini Kahama na Mchimbaji Mdogo Mwanamama Asha Hassan Msangi maarufu kama Mama Nakio wakati akizungumza na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Madini baada ya kutembelea shughuli za uchimbaji mdogo wa madini Wlayani Khama Mkoa wa Shinyanga.

Mama huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa katika uchimbaji wa madini pia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Manda Gold Mine alitoa wito kwa kina mama na wanawake kwa ujumla kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya madini huku akitolea mfano hai wa mafanikio yeke binafsi kupitia safari ya kihistoria hadi kuingia katika shughuli za uchimbaji madini na hatimaye kujizolea umaarufu mkubwa Mjini Kahama.

Mama Nakio, ambaye hivisasa anamiliki leseni 12 za uchimbaji mdogo wa madini (PML), alianza safari yake ya kibiashara katika kilimo cha mpunga. Hata hivyo, kutokana na azma yake ya kufanikiwa zaidi, aliamua kuingia kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, hatua ambayo imebadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza kuhusu safari yake, Mama Nakio ameeleza kuwa baada ya kufanya biashara ya mpunga na mchele, ilimchukua muda kidogo kufanikiwa katika shughuli zake za uchimbaji kupitia msaada wa Serikali katika kumpatia umiliki wa leseni za uchimbaji, “Kwa msaada wa Serikali, niliweza kupata leseni, jambo ambalo limenifungulia milango zaidi kwenye sekta hii ya madini,” amesema Mama Nakio, akiongeza kuwa wanawake wanayo nafasi kubwa katika kuchangia mnyororo wa thamani kwenye sekta hiyo kama ilivyo kwake.

Mama Nakio alisema kuwa, wanawake wanayo nafasi kubwa ya kubadili maisha yao kupitia sekta ya madini, huku serikali ikiendelea kuwaunga mkono kwa kuwapa fursa za kupata leseni na elimu ya uchimbaji. “Wanawake wanayo nafasi kubwa katika sekta ya madini, siyo tu kama wachimbaji bali katika mnyororo mzima wa thamani, kuanzia uchimbaji hadi usindikaji, ukiangalia hapa hapa utagundua kuwa wanawake wengi ndio wanaoongoza kutoa bei nzuri katika ununuzi wa mawe haya kabla ya kwenda kwenye krasha, na baada ya kufanya taratibu zote wanajipatia vipato vizuri tu vinavyokimu maisha yao na familia zao, pia wao ndio wanaotoa huduma za vyakula kwenye maeneo ya wachimbaji” alisisitiza Mama Nakio 

Aidha, Mama Nakio aliishukuru Serikali kwa Kuweka Mazingira wezeshi kwa watu wote kushiriki kwenye uchumi wa madini hatimaye kufanikisha ndoto zao na kubadilisha maisha yao na jamii kwa ujumla, “Kipekee tunamshuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama ametuinua sana wanawake katika kipindi hiki cha uongozi wake, tunaishukuru pia Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini, kwa kweli huyu Afisa Madini Mkazi wa hapa (Kahama) ni mwanamama mwenzetu mchapakazi na msikivu sana, anatufanya wanawake tujivunie” alisisitiza Mama Nakio.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama, Winnifrida Mrema kupitia uzoefu wake, alieleza ugumu uliokuwepo kwa wanawake kushiriki katika shughuli za uchimbaji wa madini moja kwa moja tofauti na kipindi cha sasa kwani Serikali imeweka mazingira wezeshi na rafiki kwa kila mtu kushiriki katika uchumi wa madini bila kujali jinsi yake.

“Nakumbuka wakati sisi tunaingia katika shughuli hizi za sekta ya madini, tulipokuwa tukienda kwenye shughuli za ukaguzi migodini kuna baadhi ya watu nwalikuwa wanatushangaa, lakini sasahivi idadi ya wanawake imekuwa kubwa sana katika mnyororo mzima wa shughuli za madini, kuanzia uchimbaji wenyewe, uchenjuaji na biashara ya madini, hadi watoa huduma migodini” alisisitza Mrema.

Aidha, Afisa madini huyo alimpongeza Mama Nakio kwa juhudi zake, akisema kuwa ni mfano wa kuigwa na wanawake wengine nchini na kuongeza “mfano mzuri tunao hapa Kahama, huyo Mama Nakio ameonyesha kuwa inawezekana, amejikita katika sekta hii na sasa anaendelea kufanya vizuri, kwa kweli tunawaomba wanawake wengine wajitokeze kwa wingi na kuchangamkia fursa hizi,” alisema Mrema.

Sambamba na hilo, Winnifrida Mrema alitoa rai kwa watu wote wenye leseni mbalimbali za kimadini, hususan wanawake kuzifanyiakazi leseni hizo kwa kuzingatia Sheria ya Madini na hivyo kuweza kujiimarisha kiuchumi.

Sekta ya madini imekuwa ni nguzo muhimu katika uchumi wa Tanzania, na kwa kuhusisha wanawake, inawezekana kuongeza kasi ya ukuaji na maendeleo endelevu. Kupitia ushuhuda wa Mama Nakio ameonyesha kuwa, kwa kujituma na kujiamini, wanawake wanaweza kufikia mafanikio makubwa katika sekta ambazo hapo awali zilionekana kuwa za wanaume pekee.

Serikali kupitia Wizara ya Madini iko mbioni kuzindua Programu ya Uchimbaji kwa Kesho Bora (Mining for a Brighter Tomorrow – MBT) yenye lengo la kuwajengea uwezo makundi ya kina mama na vijana wanaojishughulisha na shughuli za Uchimbaji wa Madini pamoja na mnyororo mzima wa Sekta ya Madini nchini. MBT itawasaidia Wanawake na Vijana kwa  kuwaendeleza au kuwainua kwa kuwapatia leseni  za maeneo ya kuchimba, magari, vifaa na mitambo ya uchorongaji.

 


MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali Omuka Hub  na Policy  wamezindua matokeo ya ripoti  inayoainisha uzoefu wa wanawake wa vijijini mkoani Kagera na changamoto zinazowakumba katika matumizi ya intaneti.

Uzinduzi huo ulikutanisha wawakilishi kutoka  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Wizara ya Habari, Mawasiliano  na Teknolojia ya Habari, pamoja na baadhi ya wanawake kutoka  mkoani Kagera, kujadiliana kuhusu matokeo ya ripoti na kupanga mikakati ya pamoja.

Viongozi wa mashirika ya  Omuka Hub na Pollicy,  Dorice Kaijaga  na Navina Mutabazi, walieleza mbele ya wadau  kuhusu matokeo ya kampeni yao ya siku 16 ya utafiti na mafunzo ya ujuzi kidijitali kwa wanawake wa Mkoa wa Kagera, katika mkutano uliohudhuriwa pia na maofisa wa serikali na wadau jijini Dodoma.

Kampeni yao hiyo ilijikita katika mambo ya changamoto na manufaa ya matumizi ya mitandao, pia kuwaelimisha wanawake namna bora ya kutumia mitandao hiyo kuboresha biashara zao na kupata ujuzi wa mambo mbalimbali kupitia interneti.

Walieleza kuwa utafiti huo ulifanyika mkoani Kagera kwa siku 16 za kupinga ukatili, ambapo walikutanisha wanawake 80 waishio vijijini, wanawake hao walieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili katika matumizi ya Intaneti pamoja na faida wanazozipata kupitia matumizi ya intaneti.

Baadhi ya wanawake waliowakilisha wenzao kutoka mkoani Kagera, walipata wasaa wa kuwasilisha taarifa ya kile walichokieleza, wakati mashirika haya yanafanya utafiti.

Miongoni mwa waliyoeleza ni changamoto ya upatikanaji wa mtandao wa intaneti kwa mikoa ya pembezoni, gharama za vifaa vya intaneti kuwa kubwa, uhuru wa matumizi ya intaneti kutoka kwa waume zao, pamoja na gharama za vifurushi vya simu kuwa kubwa kuliko uwezo wao.

“Mkoa wa Kagera unakabiliwa na kutokuwepo mtandao wa kutosha wa intaneti, lakini bado wanawake wengi wanakumbana na ukinzani wa wanaume kutowaruhusu kumiliki simu zenye mitandao ya kijamiii kwa mawazo ya kusalitiwa.

“Kama wanawake tunatambua fursa na mafunzo yanayopatikana kupitia simu za mkononi na tunaomba mafunzo yanayohusu umuhimu wa matumizi ya intaneti yawahusishe pia wanaume, “Esther Goldian mwakilishi wa wanawake kutoka Kagera.

Asia Abdallah kutoka Wizara ya Habari, ametoa pongezi kwa mashirikia kuona fursa iliyopo kwa wanawake na namna mashirika hayo yanavyotoa elimu kwa wanawake wa mikoa ya pembezoni, jambo ambalo litawasaidia wanawake wengi kutangaza bidhaa zao kupitia simu za mkononi na kujifunza ujuzi mbalimbali kupitia intaneti.


Wafanyakazi wanawake wa Barrick wakifurahia Siku ya wanawake baada ya kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Barrick wakikata keki kusheherekea Siku ya Wanawake duniani

****
Katika kuelekea Siku ya wanawake Duniani 2022,Kampuni ya Barrick imeandaa semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wake wanawake katika migodi ya North Mara na Bulyanhulu.