Articles by "UKAGUZI"
Showing posts with label UKAGUZI. Show all posts

 

Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bw.Diocles Ntamulyango akizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi za TBS leo Jijini Dar es Salaam.


Katika zoezi la Ukaguzi wa Magari bandarini, mpaka sasa TBS imeshakagua magari 5,445 na kati ya hayo magari 2367 yalibainika na kasoro zinazotengenezeka.

Ameyasema hayo leo Afisa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania TBS, Bw.Diocles Ntamulyango katika ofisi za shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Bw.Ntamulyango amesema katika magari ambayo yamebainika na kasoro kati ya hayo magari 1567 yamekwisha rekebishwa na kupimwa upya na yamekidhi matakwa ya viwango na yamesharuhusiwa kusajiliwa na TRA.

"Mpaka sasa tuna mashine tano ambazo zinatumika katika kukagua magari ambapo mashine nne zipo katika kituo cha TPA na mashine moja ipo katika kituo cha UDA". Amesema Bw.Ntamulyango.

Aidha Bw.Ntamulyango amesema mashine nne za kukagua magari zinauwezo wa kupima magari 496 kwa siku hivyo wanauwezo wa kupima zaidi ya magari 14,000 kwa mwezi.

Hata hivyo Bw.Ntamulyango amesema upimaji wa magari unafanyika katika vituo viwili, kituo cha kwanza kipo ndani ya bandari kipo karibu na Roro yard na kituo cha pili kipo maeneo ya UDA.

 

Mkaguzi wa TBS Bw,Sileje Lushibika akimsajili mfanyabiashara, Bw Hamza Rashid mara baada ya kukamilisha ukaguzi katika eneo la Sokoni Wilayani Sikonge-Tabora. Wafanyabiashara wanatakiwa wasajili majengo yao ili wapate kibali kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za uuzaji, usambazaji na uhifadhi wa bidhaa za chakula na vipodozi

Mkaguzi wa TBS, Bi Zena Mushi akiendelea na zoezi la usajili kwa wafanyabiashara wa bidhaa ya chakula na vipodozi katika kata ya Tatuo Wilayani Sikonge- Tabora. Wafanyabiashara hao walifurahia kusogezewa huduma hiyo na kulitaka Shirika lifanye zoezi hilo Nchi nzima

Mkaguzi wa TBS, Bw. Sileja Lushibika akiendelea na ukaguzi wa bidhaa za chakula na vipodozi sambamba na kukagua ukomo wake wa matumizi, pamoja na kusajili majengo ya bidhaa hizo katika kata ya Sikonge wilayani Sikonge-Tabora

Mkaguzi wa TBS Bw.Sileje Lushibika akiendelea na ukaguzi wa majengo ya bidhaa za chakula na Vipodozi katika eneo la Ipole, wilayani Sikonge ambapo alibani uwepo wa vipodozi vilivyokatazwa ambavyo viliondolewa kwa ajili ya kutekekezwa.


Shirika la Viwango Tanzania limeendesha program ya kukagua bidhaa ya vyakula na vipodozi Wilayani sikonge mkoani Tabora ili kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa zilizobora.

Zoezi hilo la ukaguzi limelenga pia utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu alama ya viwango kwenye bidhaa ambazo wananunua na kuuza.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika ukumbi wa Mikutano wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo tarehe 28 Machi 2021 .


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akionesha moja ya Taarifa zake za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 kabla ya kuziwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere wakati akitolea maelezo moja ya Taarifa zake za ukaguzi leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo wakati akitolea Maelezo moja ya Taarifa yake ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa mwaka 2019/20

Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga mara baada ya kutoka katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu ya Chamwino. PICHA NA IKULU.


Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Ndugu, Noely Byamungu amesema wamekamata kiasi cha Tani 4 za maziwa ya unga aina ya Miksimiksi ambayo yameiingia nchini bila vibali kwenye ghala la kiwanda cha kufungasha Maziwa ya unga aina ya Cowbell kilichopo cha Uruwira– Chang’ombe, wilaya ya Temeke kinachomilikiwa na Kampuni ya Hawaii products Supplies Limited.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ndugu Byamungu amesema walibaini ukiukwaji mkubwa wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Tasnia ya Maziwa unaofanywa na Kampuni ya Hawaii Products Supplies Limited ambayo iliingiza maziwa hayo nchini bila kupata kibali cha uingizaji wa maziwa ili kukwepa tozo.

Vilevile Ndugu Byamungu amesema katika ukaguzi huo walibaini kilo 3661.2 zimeongezewa muda wa kuisha matumizi kutoka tarehe 24.10.2021 kwakipiga chapa mpya ya tarehe ya mwisho wa matumizi ya bidhaa hizo hadi tarehe 24.8.2022 kitendo ambacho kinahatarisha usalama wa afya za walaji.

Pia, jumla ya kilo 2592 zitokanazo na ujazo wa makopo yenye ujazo wa gramu 400 kilamoja yamefungashwa upya na kutengeneza boksi (carton) 1440 zenye pakiti ndogondogo 400 kwa kila carton zimepigwa chapa ya tarehe ya mwisho wa matumizi hadi 24.8.2022.

Kutokana na utaratibu huo unaofanywa na kampuni ya Hawaii products Supplies Limited, Bodi ya Maziwa ilisimamisha shughuli zote katika kiwanda hicho baada ya kuona udanganyifu na uvunjaji wa Sheria kwa makusudi.

“ Vitendo hivi havikubaliki, havivumiliki wala kuruhusiwa kwa mujibu wa sheria, hivyo sheria itachukua mkondo wake kwa wahusika” Alisema

Mmiliki wa kampuni ya Hawaii products Supplies Limited Bw. Ahmed Suleiman pamoja Meneja uzalishaji wa Kiwanda Bw. Ahmed Amanzi waliwekwa chini ya ulinzi na uangalizi wa polisi katika kituo cha polisi cha Chang’ombe kwa ajili ya mahojiano na kukamilisha taratibu za kisheria.

 A

A     Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwenye mkutano wa uelimishajiwa zoezi la ukusanyaji wa takwimu za mifugo,kilimo na uvuvi katika Kijiji cha  Msikii, Kata ya Muhamo, Mkoani Singida hivi karibuni(Pichana John Mapepele).

B

A.      Bibi Salma Mkumbo akiuliza swali kwa wataalamu kwenye mkutano wa uelimishaji wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu za mifugo,kilimo na uvuvi katika Kijiji cha  Msikii, Kata yaMuhamo, Mkoani Singida hivi karibuni (Pichana John Mapepele).

c

A.      Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwenye mkutano wa uelimishaji wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu za mifugo,kilimo na uvuvi katika Kijiji cha  Msikii, Kata yaMuhamo, Mkoani Singida hivi karibuni(Pichana John Mapepele).

DMeneja Takwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Singida, Naing’oya Kipuyo( aliyesimama) akitoa maelezo kwa  katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi (mwenye miwani) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) kwenye ofisi ya Serikali ya kijiji cha Msikii, Kata yaMuhamo, MkoaniSingidaHivikaribuni(Pichana John Mapepele).
E
Elibariki Musa, Mkazi wa kijiji cha Msikii Kata ya Muhamo, Mkoani Singida akiuliza swali kwa wataalamu  (Pichana John Mapepele)


Na John Mapepele, Singida 

Serikali imesema takwimu sahihi zilizokusanywa kutoka kwenye sekta mbalimbali za kimkakati za Mifugo, Kilimo na Uvuvi nchini zimeifanya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Tano Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuingia kwenye Nchi za Uchumi wa Kati duniani.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na ujumbe maalum wa kitaifa ulioongozwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi wakati  walipokuwa wanakagua zoezi la kitaifa ya ukusanyaji taarifa za kina za Kilimo, Mifugo, ufugaji wa samaki Mkoani Singida ambalo  limekamilika  hivi karibuni kwa mafanikio makubwa.

“Madhumuni makuu ya Sensa hii ni kupata taarifa muhimu za kilimo, mifugo na uvuvi zitakazotumika katika kupanga na kutathmini utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya sekta katika taifa la Tanzania, na endapo ukusanywaji wa takwimu utakuwa kwenye ubora unaositahili utasaidia kulifanya taifa kupea kwenye uchumi wa juu kabisa katika kipindi kifupi kijacho” ameongeza Dkt. Chuwa

 

Akifafanua amesema taarifa  kwa mfano za magonjwa ya mifugo na mazao zitaisaidia Serikali kuainisha maeneo yanayokabiliwa na visumbufu/magonjwa  ili kuchukua hatua stahiki na kupanga mipango ya kudhibiti.Pia taarifa kuhusu uzalishaji wa mazao zitasaidia kujua kiasi cha uzalishaji kwa maeneo husika na kuiwezesha Serikali kupanga upatikanaji wa masoko na uwezekano wa kuanzisha viwanda vya kusindika mazao hayo.

 

Aidha amesema taarifa kuhusu upatikanaji na matumizi ya ardhi zitatumika kupanga mipango ya matumizi bora ya ardhi vijijini  hivyo zitatumika kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini.

 

Dkt. Chuwa ameongeza kuwa matokeo ya Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanatarajiwa kuweka msingi imara wa sekta hii kwa miaka mingi iyajo, kwa  kuwa Sekta ya Kilimo ina umuhimu mkubwa  kwenye mustakabali wa maisha ya binadamu kwa kuwa ndiyo chanzo cha chakula na malighafi zinazohitajika katika viwanda hususani katika awamu hii inayoongozwa na dira ya uchumi wa viwanda.

 

“Kutokana na umuhimu huo, na kupitia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ya Mwaka 2030, Sekta ya Kilimo ilipewa Lengo la Pili  la Kutokomeza Njaa, Kuwa na Uhakika wa Chakula, Lishe Bora na Kukuza Kilimo Endelevu. Aidha, lengo hilo limesisitiza umuhimu wa kuongeza tija katika sekta ya kilimo kwa kuongeza thamani ya mazao na pia kusisitiza matumizi bora ya ardhi na kurutubisha udongo, ili kuongeza uwezo wa binadamu kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi na athari zake yakiwemo majanga mbalimbali kama mafuriko na ukame pamoja na majanga mengine ikiwemo ndege waharibifu” ameeleza Dkt. Chuwa

   

Dkt. Lutambi amesisitiza kuwa pamoja na faida za jumla ambazo mkulima atakazozipata Sensa hii itamsaidia mtu mmoja mmoja kutatua changamoto mbalimbali katika kilimo,mifugo na uvuvi hasa upatikanaji wa pembejeo, huduma za ugani, upatikanaji wa masoko kwa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Ameongeza kuwa takwimu ni kitu cha msingi katika kupanga maendeleo kuanzia kwenye ngazi ya kijiji hadi taifa kwa kuwa zinasaidia kuonyesha changamoto na mafanikio na hivyo kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa changamoto hizo.

“Ni muhimu tukafahamu kuwa takwimu sahihi za mifugo, mazao na uvuvi zitasaidia  uchangiaji wa malighafi za  viwanda  vyetu hivyo kukuza uchumi wetu ambao tunautaka wa viwanda” amesisitiza Dkt. Lutambi

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Mohamed Bashe, kwenye hotuba yake, wakati  wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi wa Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20, iliyofanyika katika Ukumbi wa TMDA,Mwanza Julai, 25 mwaka huu alisisitiza Mwaka huu 2020, Benki ya Dunia imeitangaza Tanzania kuwa katika kundi la nchi zenye uchumi wa kipato cha kati, ambapo alisema Taarifa hizi zimeleta faraja kubwa kwa sekta ya kilimo  kwa kuwa ndiyo iliyotoa mchango mkubwa zaidi katika Pato la Taifa wa asilimia 26.6 mwaka 2019 na pia inatoa ajira kwa takribani asilimia 66 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi.

 

“Sekta ya kilimo ilichangia asilimia 24.3 ya mapato ya mauzo nje ya nchi mwaka 2019. Fedha hizi kwa kiasi kikubwa zinatumika nchini katika mambo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu wezeshi ya barabara, reli, maji, usambazaji umeme na kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za jamii kama vile afya na Elimu kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya wananchi” alifafanua Dkt. Bashe

 

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa Ripoti ya Tathmini ya Umasikini Tanzania Bara ya Mwaka 2018, sekta hii ikiendelezwa vyema ndio pekee yenye uwezo wa kuleta maendeleo jumuishi nchini, hivyo  kuna umuhimu mkubwa wa zoezi la sensa ya mifugo, mazao na uvuvi likafanyika kwa ubora na kwa umakini  unaositahili.

 

Pia wakati wa tukio la uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi wa Sensa hii, Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Amina Msengwa amesisitiza kuwa takwimu zina mchango mkubwa katika maandalizi na utekelezaji wa sera na mipango, na vile vile katika kufanya maamuzi sahihi yanayotakiwa kufikiwa kwa kutumia ushahidi stahiki (evidence based decision making).

 Amesema Sensa ya Mwaka wa Kilimo 2019/20, ni ya tano kufanyika hapa nchini tangu nchi ipate uhuru na inafanyika kwenye jumla ya maeneo yaliyochaguliwa ya kuhesabia 2,820 ambapo kutokana na maeneo hayo kaya 33,807 kutoka Tanzania bara na Zanzibar.

Kwa upande wake, Meneja Takwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Singida, Naing’oya Kipuyo ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Singida kwa kusaidia kufanikisha zoezi hili ambalo  limefanyika kwa takribani siku 50 ambapo pia amewapongeza wananchi kwa kutoa ushirikiano wa  kutosha.

 

 Kipuyo amesema taarifa zilizokusanywa kwenye Sensa hii ni za kipindi cha kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2019 hadi tarehe 30 Septemba, 2020 na kuongeza kuwa Mkoa wa Singida umekamilisha zoezi hilo kwa maeneo yote ambapo maeneo madogo ya kuhesabia watu yaani Enumaration Areas (EA) 90 yenye kaya 1087 zilizochaguliwa kwa ajili ya kufanyiwa sensa hii zilifikiwa


Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA umefanikiwa kuboresha na kusimamia uendeshaji wa Vivuko vya Serikali nchini kwa kuendelea kuongeza idadi yake kutoka kumi na tatu wakati wakala ukianzishwa 2005 hadi kufikia thelathini pamoja na boti ndogo tano.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji mkuu wa TEMESA  nchini Mhandisi  Japhet Maselle wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ,ambapo amesema idadi hiyo ni ongezeko la vivuko kumi na saba.

“Wakala kwa sasa inatekeleza ujenzi wa vivuko vipya kwa ajili ya maeneo ya Mafia-Nyamisati  ambao unagharimu  Bilioni 5.3 ,Bugorola –Ukara  Bilioni 4.2,Chato-Nkome unagharimu Bilioni 3.1 na Kayenze –Bezi Tsh.Bilioni 2.7.Ujenzi wa Vivuko vyote hivi unagharimu fedha za
Kitanzania Tsh.Bilioni 15.3.”amesema.

Mhandisi Maselle amesema TEMESA kwa kushirikiana na Wizara wanaandaa mfumo wa TEHAMA ili kudhibiti uzito wa abiria na mizigo inayobeba na pia kuhakikisha usalama wa mali.

“TEMESA pia imejipanga ufungaji wa vifaa vya TEHAMA  ikiwa ni pamoja na CCTV Camera kwa ajili ya Usalama na kurahisisha ufanyaji kazi,mfano kuna kuandaa mfumo wa wa usimamizi na ufuatiliaji wa mienendo ya vivuko kwa kudhibiti uzito  wa abiria na Mizigo inayobebwa  kwenye
vivuko[Ferry Management System]”Amesema.

Aidha amegusia juu ya uboreshaji wa karakana za kutengeneza magari ya Serikali ambapo amesema kuwa hadi sasa wakala huo una karakana 26 katika Mikoa yote ya Tanzania na vifaa vyote vikiwemo vipuri vipo vya
kutosha kwa ajili ya kazi.

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA ulianzishwa chini ya Sheria ya Wakala namba 30 ya mwaka 1997 ambapo ilikasimiwa karibu majukumu yote yaliyokuwa yanatekelezwa na Idara ya Ufundi na Umeme chini ya Wizara ya miundombinu, lengo likiwa kutoa huduma bora katika Nyanja za Uhandisi mitambo,umeme,Elektroniki na Uendeshaji Vivuko.



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Diwani wa Viti Maalumu kwa tiketi ya CHADEMA kata  ya Maruvango  Digna John Nassari ameamua kushirikiana na wananchi ,wadau wa maendeleo pamoja na Viongozi wa CCM katika kukarabati na kufungua barabara za vijiji vilivyopo katika kata hiyo ambazo zilikua hazipitiki kwa kipindi kirefu na kusababisha adha kubwa hasa kwa wananchi hususan wagonjwa na wakinamama wajawazito kushindwa kufika katika huduma za afya kwa  wakati na hata kupoteza maisha.

Akizungumzia ukarabati huo Diwani huyo amesema kuwa  baada ya kuona adha wanayoipata kinamama kwenda sokoni na kufikia vituo vya afya wameamua kufungua barabara hizo ambazo baadhi zilikua katika hali mbaya ya kutokupitika kabisa lakini kwa sasa wameweza kuzifungua barabara hizo upya na wananchi wanapita bla shida.

Digna  amesema kuwa ameshirikiana na wananchi pamoja na wadau ambao wamechangia mafuta ya katapila,greda la kushindilia ambalo ni mali ya Halmashauri ya Meru  pamoja na fedha za kuwalipa madereva huku msaada mkubwa ukitoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Meru Jerry Muro pamoja na Wenyeviti wa vijiji ambao wengi wao ni wa CCM lakini kwa hili  wameshirikiana vyema kufanikisha ukarabati wa barabara.

“Niliwaita rafiki zangu nikawaomba wanichangie fedha kwa ajili ya mafuta kwa ajili ya magreda ambayo ,kampuni ya Arusha Agrigates walinipa mafuta lita 50,kampuni ya Lake Oil iliyopo maji ya Chai walinipa lita 100,King`ori Agrigates lita 100,Munio walinipa lita 50 kwa kweli nawashukuru sana wadau wa maendeleo kwa kunisaidia pia  Dc Muro alinisaidia kupata barua ya kuomba mchango wa wadau pia viongozi wa Vijiji wamenipa mafuta kwa ajili ya katapila”

Afisa Mtendaji wa Kata ya Maruvango Hassan Shomari Kupe amesema kuwa miaka ya nyuma barabara zilikua nyembamba hazipitiki zilikarabatiwa mwaka 1950  hata kinamama wajawazito walipata tabu kwenda kwenye zahanati ,lakini kwa sasa Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano Raisi Magufuli,Mkuu wa Wilaya na Diwani kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha adhma hii ya kuwatumikia wananchi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbaseny Zablon Lucas amepongeza juhudi zilizofanywa na Diwani huyo ambazo zimewezesha barabara kupitika kwa urahisi hasa kwa wakulima kusafirisha mazao yao kuyapeleka masokoni.

Elly Elirehema Urio amesema kuwa barabara hiyo itakua mkombozi kwa kinamama kwani miaka mingi waliteseka na hawakupata barabara ila kwa sasa wana uhakika wa kuwa na barabara zitakazopitika kwa kipindi chote cha mvua na jua.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uko pale pale na utafanyika Novemba 24, 2019 kama ilivyopangwa licha ya vyama vingine kujitoa kwenye Uchaguzi huo.

Jafo ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Ofisini kwake Jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya  maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea uongozi sambamba  na Kamati za Rufaa.

Alisema zoezi la uchukuaji wa urejeshaji wa fomu za kugombea uongozi limeenda vizuri na wananchi waliochukua fomu ni 555,036 na waliorejesha ni 539,993 sawa na asilimia 97.29 ya wananchi wote waliochukua fomu, na ambao hakurejesha ni asilimi 2.7 tu.

“Hii inaonyesha muamko mkubwa wa wananchi kutaka kuongoza katika ngazi ya Serikali za Mitaa na mchakato mzima wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu ulienda vizuri ukiwa na Kanuni bora zaidi  kulinganisha na chaguzi zilizotangulia” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa baada ya zoezi hili kukamilika lilifuatiwa na uteuzi ambao ulilenga kuteua wagombea wenye sifa, waliokidhi vigezo na kufuata taratibu zote za ujazaji wa fomu za kugombea na kubandiwa kwa orodha ya wagombea waliopitishwa katika hatua hiyo.

Wagombea pia walipata fursa ya kuwasilisha pingamizi zao kwa mujibu wa Kanuni na kisha kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa za Wilaya zilizoundwa kwa ajili ya kuratibu rufaa za wagombea alisema Jafo.

Waziri Jafo alifafanua kuwa mpaka hivi sasa rufaa zilizowasilishwa kutoka kwenye vyama mbalimbali vya siasa ni 13,500 na zinafanyiwa kazi na Kamati za Rufaa za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo zoezi hilo litakamilika leo hii Tarehe 09/11/2019.

Akizungumzia baadhi ya vyama kujitoa kwenye Uchaguzi ilihali wanachama wao walishateuliwa amma kuwasilisha rufaa zao kwenye Kamati  alisema kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi jina la mgombea likishateuliwa linabaki kwenye karatasi za kupigia kura siku ya Tarehe 24/11/2019 hata kama chama chake kimejiengua kushiriki kwenye Uchaguzi .

Aliendelea kuelezea kuwa wakati zoezi la uteuzi na kamati za rufaa zikiendelea na kazi yake alipata fursa ya kufanya ziara katika mikoa ya Singida, Manyara, Dododma,Iringa na Njombe ambapo  alijionea baadhi ya makosa yaliyofanywa na wagombea wakati wa ujazaji wa fomu lakini pia alizungumza na Kamati za Rufaa.

Alitaja makosa yaliyobainishwa kwenye fomu za wagombea kuwa ni  “Kujaza umri mdogo kuliko umri unaostahili kwa mgombea, sehemu ya tarehe kuweka sahihi au mtu kuchukua fomu na kujidhamini mwenyewe au majina kutofautiana wakati wa kujiandikisha kwenye orodha ya mpigakura na kwenye fomu ya kugombea hivyo Wasimamizi walifanya kazi yao kwa mujibu wa miongozo na Kanuni za Uchaguzi” Alisema Jafo.

Lakini bado nafasi ilikuwepo endapo mgombea  angeona hakuteuliwa kwa kuonewa ipo Kamati ya Rufaa ambayo ingeweza kuskiliza malalamiko ya mgombea na kuyafanyia kazi alisisitiza Jafo.

“Kuanzia kesho tutaanza kutoa Taarifa ya Rufaa zilizopita na watu walioteuliwa kushiriki uchaguzi huo kupitia Kamati za Rufaa " alimalizia Waziri Jafo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila leo  Septemba 2,2019 ameongoza kufanya ukaguzi maalumu kwa madereva wa Bajaji wenye leseni Jijini Mbeya ,ukaguzi huo umehusisha Jeshi la Polisi

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Tanesco mkoa wa Arusha imefanya Operesheni Maalumu ya kukagua mita zaidi ya 1000  na kubaini  baadhi ya watu waliochakachua mita za umeme ikiwa ni njia ya kukwepa kulipa malipo stahiki ya huduma za umeme hivyo wamechukuliwa hatua za kisheria.

Afisa Ukaguzi wa Mita  Zuberi Hassan amesema kuwa baada ya kufanya ukaguzi huo wamebaini mita kadhaa ambazo zimechezewa ili zisiweze kusoma vizuri matumizi ya umeme jambo ambalo ni hujuma kwa shirika hilo.

Mmiliki wa eneo ambalo lilikaguliwa na kukutwa na tatizo la mita kuchakachuliwa ,Joseph Shirima   amesema kuwa tatizo hilo lilisababishwa na baadhi ya wapangaji wasio waaminifu kufunga mita zao hivyo atashirikiana na shirika hilo ili kuhakikisha mita zinazowekwa zina kuwa na usahihi.

Meneja wa wateja wakubwa Tanesco  Mhandisi Frederick Njavike  amesema kuwa shirika hilo limefanya ukaguzi wa mita zaidi ya 1000  katika maeneo mengi jijini Arusha ili kujiridhisha na mita zilizopo pamoja na kuchukua hatua stahiki ikiwemo kusitisha huduma za umeme pamoja na kuchukua hatua Kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wateja wenye tabia ya kuchezea mita

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiongea na waandishi wa habari juu ya kuridhishwa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya kilolo mkoani Iringa 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akieleza jinsi gani atakavyo hakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi wa wanaojenga hospitali hiyo ili kusitokee kasoro zozote zile
 Haya ni baadhi ya majengo yaliyojengwa katika hospitali ya wilaya ya kilolo mkoani Iringa ambayoWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wake

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa unaotekelezwa kwa kutumia  zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukagua hospitali hiyo Waziri Jafo amesema kuwa kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo inaridhisha na baada ya kukamilika kwake itawasaidia wananchi wengi wa maeneo hayo pamoja na kupunguza msongamano katika hospitali ya rufaa.

“Niwahakikishieni viongozi wa wilaya na mkoa kuwa nimeridhishwa na kasi hii ya ujenzi wa hospitali hii kwa kuwa mnasimamia vilivyo kwa kuhakikisha fedha za serikali zinatumia vizuri hivyo niwapongeze sana” alisema Jafo

Jafo alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano ipo makini katika kuhakikisha wananchi wa chini wanapata huduma muhimu bila kizifuata kama ilivyokuwa awali na amehaidi kuwa atazifukisha salamu kwa Mheshimiwa Rais juu ya hatua ambazo zinaendelea katika hospitali hiyo

“Leo naweza kuwapongeza mmefanya kazi kubwa ya kusimamia ujenzi huu ambao umekuwa ukienda vizuri kila hatua ambayo nimekuwa nikifuatia hatua kwa hatua hadi hii leo naona matunda yake” alisema Jafo

Aidha Jafo aliwataka viongozi kuhakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi wa majengo hayo kumalizia vizuri ili kuondokana na kasoro mbalimbali ambazo zimekuwa zimejitokeza hasa kwenye milando bado kunashida kuhatajikajia kurekebishwa.

“Nimetembea kwenye majengo haya yamejengwa vizuri kwa kufuata vigezo stahili lakini tatizo ambalo nimelibaini ni kuwa mirango haijakaa vizuri inahitajika kutolewa na kuwekwa milango mipya hivyoa naombeni hakikisheni mnasimamia” alisema Jafo

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alisema kuwa wataendelea kuwasimamia wakandarasi hao ili kuhakikisha wanarekebisha kasoro zote ambazo zimejitokeza katika hatua hizo za umaliziaje wa ujenzi huo wa hospitali hiyo ya wilaya ya Kilolo.

“Mheshimiwa waziri tumezipokea pokea kasoro hizo ambazo umetuagiza tumsimamie waha wakandarasi na sisi tutazisimamia vilivyo ili kupata hospitali iliyo bora kwa kila kitu na kuwa mfano wa kuigwa kwa hospitali nyingine” alisema Hapi

Hapi alimuomba waziri Jafo kuhakikisha anawafikishia shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kwa kuwapa fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya mkoa wa Iringa.

“Kwa kweli tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kuendelea kutuletea fedha kwenye miradi mingi ya kimkakati hivyo tunashukuru sana” alisema Hapi

Naye mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa atahakikisha kila uchwao anaendelea kusimamia ujenzi wa hospitali hiyo kwa kuwa ipo katika wilaya yake.

“Mimi nitaendelea kusimamia kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kila kitu kinaenda kama ilivyokusudiwa na kuwa hospitali ya mfano hata nchini hivyo nikuahidi nimeyachukua kwa umakini mkuwbwa maagizo yako” alisema Abdalah

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa kamati ya maaandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi za Mei Mosi walipokutana nao kukagua maandalizi hayo katika Viwanja vya  Sokoine Jijini Mbeya Aprili 29, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na kamati ya maaandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi za Mei Mosi walipokutana nao kukagua maandalizi hayo katika Viwanja vya  Sokoine Jijini Mbeya Aprili 29, 2019.
 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.

Mjumbe Kamati ya Utendaji CWT Mwalimu Joyce Julius akichangia jambo katika kikao cha maandalizi ya sherehe za Mei Mosi kilichofanyika katika Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya aprili 29, 2019.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiangalia mazingira ya uwanja wa Sokoine utakaotumika kwa ajili ya Maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi kitaifa Jijini Mbeya alipokutana na kamati ya maandalizi ya sherehe hizo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati wakiwa katika ukaguzi wa maadalizi ya sherehe za Mei Mosi katika viwanja vya Sokoine Mkoani Mbeya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na kamati hiyo wakiangalia mtaro unaopitisha maji katika viwanja vya Sokoine ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufikia Kilele cha Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) Jijini Mbeya.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu maendeleo  ya ujenzi wa kituo cha Mizani kinachojengwa Dakawa Mkoani Morogoro, wakati kamati hiyo ilipokagua mzani huo. Wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Suleiman Kakoso.
????????????????????????????????????
Mafundi wa Kampuni ya Group Six International wakiendelea na ufungaji wa Kamera katika mzani mpya unaojengwa eneo la Dakawa mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Muonekano wa jengo la mzani mpya unaojengwa Dakawa Mkoani Morogoro. Mradi huo umekamilika kwa asilimia 98.
????????????????????????????????????
Mhandisi Mshauri Kasmir Mustapha (kulia), akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu maendeleo  ya ujenzi wa kituo cha Mizani kinachojengwa Dakawa Mkoani Morogoro, wakati kamati hiyo ilipokagua mzani huo.
………………………
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kujenga nyumba za watumishi kwenye mzani mpya unaojengwa Dakawa Mkoani Morogoro ili kuwapunguzia adha wafanyakazi watakaokuwa wakifanya kazi kituoni hapo.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Sulemani Kakoso ameipongeza Wizara na kuhakikisha kuwa pamoja na kujengewa nyumba hizo, pia Wizara iwasimamie watumishi wa mzani vizuri ili kuepuka vitendo vya rushwa.
“Serikali imetumia fedha nyingi kujenga mzani huu, nawapongeza sana lakini sasa ni muhimu watumishi wa mzani huu wakasimamiwa vyema ili kuepuka vitendo vya rushwa vinavyofanywa na watumishi wasio waaminifu” amesema Mwenyekiti. Kakoso.
Mwenyekiti Kakoso, ametoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini kuhakikisha wanazingatia sheria za mizani kwa kupakia mizigo isiyozidi kiwango ili kulinda miundombinu ya barabara nchini.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha changamoto zote zilizowasilishwa zinatatuliwa mapema ili kuongeza ufanisi.
Naibu Waziri huyo ameieleza kamati hiyo kuwa ujenzi wa mzani huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 14.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Mazingira kutoka Sekta ya Ujenzi Mhandisi Julius Chambo, amesema ujenzi wa mzani huu unatokana na mzani wa Kihonda kuzidiwa na msongamano wa magari kwa kuwa ni wa upande mmoja.
Ameeleza kuwa ukamilikaji wa mzani huu utasaidia kuokoa muda kwa wasafirishaji na kuondosha msongamano uiopo sasa katika mzani wa Kihonda kwani mzania huu utapima tu yale magari yanayoonekana yamezidi uzito tu.



JENGO%2BWIZARA%2B2
Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.
WAKIKAGUA%2B%2B1
Waziri wa Madini Doto Biteko, (mwenye koti) Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) na Prof. Simon Msanjila (mwenye tisheti nyekundu) wakikagua maeneo maeneo mbalimbali ya jengo la Wizara
WAKIKAGUA%2B%2BMAENEO%2BMBALIMBALI
Waziri wa Madini Doto Biteko ( wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto ) na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila, wakijadiliana jambo wakati wakikagua maeneo mbalimbali ya jengo la Wizara, eneo la Ihumwa.
WAKITAZAMA
Waziri wa Madini Doto Biteko katikati na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakiangalia kitu wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara, Ihumwa.
…………………….



*Viongozi Waandamizi Madini watembelea jengo la Wizara, Ihumwa
*Waziri Biteko asema wizara iko tayari kuwahudumia watanzania kutokea Ihumwa
*Mkandarasi aahidi kukamilisha ujenzi ndani ya siku Tano

Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini, wakiongozwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko  wametembelea Jengo la Wizara ya Madini lililopo mji wa Serikali eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi huo.

Akizungumza baada ya kukagua jengo hilo, Waziri wa Madini Doto Biteko amewahakikishia watanzania wote pamoja na wadau wa madini kuwa, wizara iko tayari kuwahudumia kutokea eneo hilo la Ihumwa pindi itakapohamia na kuwataka watumishi kujiandaa kuhamia eneo hilo mara baada ya mkandarasi kukabidhi jengo kwa wizara. Vilevile, Waziri Biteko amezitaka taasisi nyingine zenye uhitaji wa kutumia madini ya mawe yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na mable, kuwa wizara iko tayari kuwasaidia kwa kuwaunganisha na wajeta wake.

Pia, amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutokana na msukumo alioutoa kuhakikisha ujenzi wa majengo ya serikali unakamilika kwa wakati. Aidha, amempongeza Mkandarasi kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd kutokana na kuongeza kasi ya ujenzi ikiwemo kuzingatia ubora nakuongeza kwamba, wizara imeridhika na ujenzi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameeleza kuwa, wizara imepanga kulifanya eneo la ofisi hiyo kuwa kijani kwa kuhakikisha inapanda miti ya aina mbalimbali na kuhakikisha kwamba eneo hilo linawekewa mazingira mazuri ya kuvutia. 

Naye, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila Amesema Mkandarasi Kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd imeahidi kuikabidhi Wizara jengo hilo ndani ya kipindi cha siku Tano zijazo “awali ujenzi ulianza kwa kusuasua lakini sasa uko katika hatua nzuri na mkandarasi amezingatia ubora,” amesema Prof. Msanjila. 

Akizungumzia mahitaji ya ofisi na idadi ya watumishi, amemsema kwa idadi ya watumishi wa wizara Makao Makuu ofisi zilizopo katika jego hilo zinatosheleza mahitaji na kuongeza kuwa, kwa kuanza Idara zote na Vitengo vya Wizara vinatarajia kuhamia katika eneo hilo isipokuwa Idara ya fedha kutokana na masuala ya mfumo wa kifedha. Pia, ameeleza kuwa, wizara imetumia malighafi inayopatikana nchini yakiwemo madini ya mable ambayo yamepatikana kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini.

Kwa upande wake, Mkandarasi wa kampuni hiyo Hamisi Msangi ameihakikishia wizara kuwa , ndani ya siku tano zijazo, jengo hilo litakabidhiwa rasmi kwa wizara hiyo.
 Meneja wa Shirika la umeme, TANESCO mkoa wa Rukwa, Frank Chambua (kushoto), akitoa maelezo kuhusu upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme katika mkoa huo kwa viongozi wa bodi ya Tanesco nchini walioongozwa na makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Dkt. James Nzagi, (mwenye shati ya mabaka) mara baada ya kutembelea kituo  cha kupooza umeme kilichopo eneo la majengo mjini Sumbawanga. 
Meneja wa Shirika la umeme TANESCO mkoa wa Rukwa, Frank Chambua (kulia), akitoa maelezo kuhusu upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme katika mkoa huo kwa viongozi wa bodi ya Tanesco nchini walioongozwa na makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi James Nzagi, leo mara baada ya kutembelea kituo  cha kupooza umeme kilichopo eneo la majengo mjini Sumbawanga. 
 Mdhibiti mifumo ya umeme wa TANESCO mkoa wa Rukwa, Halfan Seba (kulia), akitoa maelezo  kuhusu uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme katika mkoa huo kwa viongozi wa Bodi ya Tanesco nchini walioongozwa na Makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi James Nzagi, leo mara baada ya kutembelea kituo hicho kilichopo eneo la majengo mjini Sumbawanga.
 Mdhibiti mifumo ya umeme wa TANESCO mkoa wa Rukwa, Halfan Seba (kulia), akitoa maelezo  kuhusu uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme katika mkoa huo kwa viongozi wa Bodi ya Tanesco nchini walioongozwa na Makamu mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi James Nzagi, leo mara baada ya kutembelea kituo hicho kilichopo eneo la majengo mjini Sumbawanga.
 Makamu mwenyekiti wa bodi ya shirika la umeme nchini (TANESCO), Balozi Dkt. James Nzagi  akiambatana na wajumbe wengine wa bodi hiyo kukagua eneo lililotengwa kwa ajili ya  kujengwa kwa kituo cha kupoza umeme wa gridi ya taifa mkondo KV 411 lililopo katika kata ya Malangali mjini Sumbawanga Machi 11, 2019 wakati wa ziara ya viongozi wa bodi hiyo mkoani hapa kukagua miundombinu ya Shirika ikiwa ni pamoja na kuangalia hali ya upatikanaji wa umeme.
 Makamu mwenyekiti wa bodi ya shirika la umeme nchini (Tanesco), Balozi Dkt. James Nzagi (katikati), akitoa maelekezo kwa watendaji wa shirika hilo mkoa wa Rukwa mara baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha na kusambaza umeme cha mjini Sumbawanga wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya shirika hilo.
Makamu mwenyekiti wa bodi ya shirika la umeme nchini (Tanesco), Balozi Dkt. James Nzagi (kulia), akitoa maelekezo kwa watendaji wa shirika hilo mkoa wa Rukwa mara baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha na kusambaza umeme cha mjini Sumbawanga wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya shirika hilo.