Articles by "MEYAARUSHA"
Showing posts with label MEYAARUSHA. Show all posts

 



Jiji la Arusha limezindua mitambo yenye thamani ya bilioni 1.7 itayotumika kutengeneza miundombinu ya barabara zisizokidhi vigezo kwa mujibu ya taratibu za TARURA katika kata zake 25 na mitaa 154.

Akizindua mitambo hiyo ambayo ni Katapila lenye thamani ya zaidi ya bilioni 1 na Malori mawili yenye thamani ya zaidi ya milioni 413 Meya wa jiji hilo Maxmilian Irange
alisema kuwa barabara zitakazohudumiwa na mitambio hiyo ni zile za mita 4 mpaka sita ambazo wakala wa barabara vijijini (TARURA) haiwezi kuzihudumia.

Alisema kuwa pesa zilizotumika kununua mitambo hiyo nifedha za mapato ya ndani ya halmashauri hivyo wote kwa pamoja waitunze na ikitokea kuna ujanja wowote wa kuchepusha mitambo hiyo kwenda kwenye shughuli zisizo rasmi watoe taarifa.

"Mitambo hii kwa mujibu wa taratibu za manunuzi ina muda wa uangalizi l(warranty) lakini tukiitunza tunaweza kuitumia hata miaka kumi kwahiyo barabara zetu tuna uhakika zitakuwa kwenye hali nzuri kwa miaka yote hii cha muhimu ni tushirikiane kutunza"Alisema Meya Irange.

Aidha aliwataka madiwani kuainisha barabara hizo ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wananchi kutojenga katika hifadhi za barabara ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira kwa kupanda ili kuepuka ukame.

Kwa upande wake mmwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Wilfred Soilel aliwataka viongozi wa halmashauri pamoja na madiwani wote kuwa waangalifu katika kusimamia hasa wakati zinapokuja taarifa za kuharibika ili kuhakikisaha vifaa vilivyoharibika ni kweli lakini pia kuzuia kubadilishwa kwa vifaa.

"Tunafahamu kuwa barabara zetu za mitaa TARURA hawawezi kuzihudumia hivyo kwa uamuzi huu wa kununua hii mitambo ninawapongeza sana lakini ninaomba mvitunze isije ikafanya kazi kidogo mkasema vimeharibika na ikitokea imeharibika mjiridhishe ni kweli imeharibika msije mkabadilishiwa vifaa vikawekwa vibovu alafu mkaambiwa imeharibika, wanachi wakaendelea kuteseka na ubovu wa miundombinu.

Naye mkurugenzi wa jiji la Arusha John Kayombo alisema kuwa walitenga bilioni 2 hivyo fedha iliyobaki itatumika kununua vifusi kwaajili ya matengenezo ya barabara ili wananchi waweze kupita sehemu nzuri na hakuna diwani ataye pitishwa kwenye maji tena kutokana na changamoto ya barabara.

"Huu mtambo utaenda kushughulika huko na kuhakikisha kwamba magari, bodaboda, guta na wananchj wenyewe watapita bila changamoto" Alisema Mkurugenzi.

 


Baraza la Madiwani Jijini Arusha wamechachamaa wakihoji kwa nini miradi ya ujenzi wa barabara na uwekaji wa mitaro imeshindikana kukamilika hadi mvua zimeanza kunyesha, hatua inayopelekea madiwani kutoaminika kwa wananchi wao. 

Wameibua hoja hiyo katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025, wakihoji juu ya fedha zilizotengwa milioni 28 kwa kila kata kutengeneza miundombinu hiyo, na kutaka majibu yenye ufafanuzi kutoka kwa mwenyekiti wa baraza juu ya jambo hilo ambalo linawakosesha imani na wananchi wao. 

Diwani wa viti maalum Sakina Mpanju, Isaya Doita wa Ngarenaro, Labora Ndarpoi waTemi, Naboth Silasie wa Lemala ni baadhi ya madiwani waliotaka ufafanuzi kwa nini miradi ya barabara imeshindikana kukamilika kwa wakati ilihali pesa zimeshatengwa. 

"Sisi ndio tunaona adha wanayopitia wananchi, kama kipindi hiki mvua zinavyoendelea kunyesha mitaro imeziba na barabara zinazidi kuharibika, wananchi wanashindwa kufanya shughuli zao kwa uhuru kwa sababu ya ubovu wa miundombinu, tunaomba majibu ya uhakika ya kuwapa wananchi wetu" wamehoji Madiwani hao. 

Awali akifungua baraza hilo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe amedokeza akiwataka madiwani hao kutojadili suala la barabara kuwa, vifaa vimeagizwa vikifika wataambiwa. 

"Vifaa vimeagizwa nje na vikiletwa tutaitana kuvipokea ili kazi ya matengenezo ya barabara na mitaro iendelee, bahati nzuri ukusanyaji wa mapato unaenda vizuri, hivyo ni imani yangu kwamba miradi yote itakamilika kwa wakati" ameeleza Iranqhe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa akizungumza katika baraza hilo amewataka watendaji wote wanaohusika na miradi ya barabara wakiwemo TARURA na Watu wa manunuzi, kuikamilisha kwa wakati vinginevyo wataachia nafasi zao. 

"Nawaambia madiwani muda wenu ni mchache, acheni kuwachekea hawa watawaangusha shimoni, muda ukifika mtaogopa kusimama majukwaani kunadi sera zenu kw sababu ya wazu wazembe wanaopokea fedha na kushindwa kuwajibika ipasavyo, maana wananchi wanawaangalia nyinyi, endeleeni kufumbia macho mambo haya mtaumia"ameongeza

" Kama hizo pesa zimeshatengwa ni miezi mitatu sasa kwa nini changamoto ziko palepale, sitamvumilia yeyote atakayetaka kurudisha nyuma jitihada za serikali" ameeleza Mtahengerwa. 

Hata hivyo amewakumbusha madiwani kusimamia usafi wa mitaa, kuhamasisha ufungaji wa taa za barabarani, kupanda miti na kuibua wanaojihusisha na utengenezaji wa pombe haramu.

 

Meya wa Jiji la Arusha Maximillan Iraghe akishiriki Mbio za Clock Tower Marathon na kukimbia mbio hizo  kilomita 10 zilianzia na kuishia kwenye uwanja wa Gymkana Jijini Arusha.


Meya wa Jiji la Arusha Maximillan Iraghe amewataka waratibu wa mbio za Clock Tower kuzifanya mbio hizo kuwa za kipekee zinazokimbiwa ndani ya Jiji la Arusha ili kuhakikisha wanaendelea kulitangaza vyema Jiji la Arusha  pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kuhifadhi na kutunza mazingira kwenye vyanzo vya maji vinavyolizunguka Jiji hilo.

"Niendelee kuwasihi wadau wa utalii katika Jiji letu sambamba na wananchi wote waendelee kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wanatekeleza mipango ya kuimarisha shughuli za uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji". Alisema Iraghe

Sambamba na hilo ameendelea kuwakumbusha wananchi wa Jiji la Arusha kuwa asilimia 45 ya wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali zilizopo ndani ya Jiji hili  ni wenye magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo, kisukari na kwamba njia mojawapo ya kuzuia matatizo hayo ni kufanya mazoezi.




KATIKA kufanikisha mkakati wake wa kufanikisha usambazaji wa nishati ya jua nchini na bidhaa bora zinazotumia nishati hiyo, kampuni ya Sun King imefungua ofisi zake mkoani Arusha.

Hafla ya uzinduzi wa ofisi hizo ulihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Mauzo wa Sun King, Victor Agandi, Meya wa Jiji la Arusha, Mhe. Maximilian Iranghe na wageni mbalimbali.

Meya Iranghe, aliipongeza Sun King kwa kujitolea kwa jamii, kwa kutoa mtambo wa kisasa wa umeme wa jua (Solar Inverter) sambamba na kuadhimisha uzinduzi.Mtambo huo wa kusambaza umeme wa jua wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 7,000,000 uliofungwa utawezesha maabara ya kituo cha afya cha Themi kilichopo jijini Arusha kufanya kazi na kusambaza umeme kwenye wodi ya akina mama, na hivyo kuimarisha utendaji kazi wa kituo hicho na jamii kupata huduma bora za afya.

Mfumo huu wa kibunifu wa umeme jua, ni mojawapo ya bidhaa za hivi karibuni za Sun King, umeundwa kushughulikia matatizo mengi ya nishati hapa nchini Tanzania. Tunaahidi kuendelea kupunguza gharama kubwa za nishati kuanzia kwenye kaya za mijini na biashara kwa ujumla.

"Ninayo furaha kusikia kwamba Sun King hivi karibuni ilitunukiwa Tuzo ya Kampuni Bora ya Mwaka ya Watoa huduma za Bidhaa za umeme wa jua katika Tuzo za Kampuni Bora ya Afrika," alisema Meya Iranghe. "Sifa hii inadhihirisha kuwa mnavyo vigezo vya kutoa huduma zenu nchini na Afrikai, ikithibitisha dhamira ya Sun King ya kusaidia kuleta maisha bora kwa mamilioni ya watu ulimwenguni kote."

Akitoa shukrani zake kwa wageni na wafanyakazi wa Sun King Tanzania, Victor Agandi, Makamu wa Rais Mauzo ya huduma za Nishati ya jua kwa mfumo wa gharama nafuu kwa wateja kwa Afrika Mashariki na Kusini, alisema, "Hili ni tukio muhimu kwa Sun King Tanzania. Ninajivunia mafanikio yetu na ninashukuru kwa matokeo chanya tuliyoleta Tanzania na Afrika kwa ujumla. Tunaendelea kuwa thabiti katika dhamira yetu ya kutoa suluhisho la nishati ya jua kwa bei nafuu, kuaminika na endelevu kwa wale walengwa.

Kujitolea kwa Sun King kwenye uvumbuzi na matokeo chanya kwenye kijamii kumeiweka kama kiongozi kwenye tasnia. Dhamira ya kampuni ya kuendelea kupeleka nishati safi kwa watanznaia ambapo mpaka sasa watanzania takribani milioni mbili wamefikiwa na nishati hii. Sun King inaendelea na safari yake ya kuleta matokeo chanya na bora, kukuza maendeleo endelevu na ustawi duniani kote. Kampuni imepata tuzo nyingi na sifa kwa ufumbuzi wake wa ubunifu kwa changamoto za upatikanaji wa nishati, ikiwa ni pamoja na kutambuliwa kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa, S & P Global Platts, tuzo ya Ashden na tuzo ya Global LEAP kwa kutaja chache.

Shughuli za Sun King zimesambaa katika nchi nyingi barani Afrika, zikiwemo Cameroon, Kenya, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Tanzania, Togo, Uganda, na Zambia. Sun King inatoa huduma zake kwa kushirikiana na wasambazaji wa ndani, taasisi ndogo za fedha, na mashirika yasiyo ya kiserikali katika nchini za Afrika ili kufikia jamii mbalimbali zisizounganishwa za gridi ya Taifa.