Articles by "Ajali"
Showing posts with label Ajali. Show all posts

 Na Oscar Assenga, Handeni.



WATU 11 wamefariki dunia wa Kijiji cha Chang’ombe kilichopo Kata ya Segera wilayani Handeni Mkoani Tanga baada ya kugongwa na lori lililokuwa limebeba saruji baada ya kupoteza uelekeo wakati walipojitokeza barabarani walipokuwa wakishanga ajali ya gari dogo aina ya tata .

Watu hao walijitokeza barabarani ili kuweza kutoa msaada kufuatia ajali ya barabarani ya gari dogo aina ya Tata ndipo walipokumbana na ajali hiyo iliyopelekea kupoteza maisha..

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian lori hilo liliwagonga watu hao usiku wa kuamkia Januari 14,2025 na kusababisha vifo hivyo pamoja na majeruhi.

Lori hilo lenye namba za usajili T.680 BQW likiwa linatokea Tanga lilifeli breki na kuwagonga watu waliokuwepo pembezoni mwa barabara na kusababisha vifo vya watu 11 papo hapo na kujeruhi wengine 11.

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Korogwe Magunga na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo .


Hata hivyo Mkuu wa Mkoa huyo alitoa pole kwa familia za marehemu na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi wote .

Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali nzuri ya kiufundi ili kuepusha ajali za namna hiyo.


 

Wafanyakazi wa Benki ya Amana wakijaribu matumuzi ya Apps hiyo wakati wa uzinduzi  wa programu yake mpya ya kidigitali ijulikanayo kama Amana Bank App ambayo itawawezesha wateja kufanya miamala mtandaoni.
***
Aliyekuwa Katibu Tawala (DAS) Boniface Maiga Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga amepoteza maisha katika ajali huku watu watatu wakijeruhiwa akiwemo Mbunge wa Jmbo la Handeni Omary Kigoda ambaye amevunjika vidole viwili vya mkono wa kulia wakati wakielekea kwenye mkutano mkuu jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa yake dereva wa gari la Mbunge wa Handeni Omary Kigoda, Peter Mganga amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa saba usiku katika eneo la Vikonji Dodoma.

Amesema chanzo cha ajali hiyo imetokana na mwendokasi aliokuwa dereva wa basi baada ya kulipita sehemu yenye kona kitendo ambacho si sahihi.

Dereva huyo wa mbunge amesema baada ya dereva wa basi kulipita katika eneo hilo lenye kona kali alimuwashia taa ili aweze kupunguza mwendo gari ila dereva wa basi hilo hakupunguza spidi na ndipo wakavana uso kwa uso.

“Katika ajali hii dereva na kondakta wa basi wote wamefariki nilijaribu kumwashia taa nyingi ili apunguze spidi lakini cha kushangaza kama hajaziona ilibidi sisi tupaki pembeni ndipo mwendo aliokuwa nao ililazimu kulivaa gari letu hasa upande wa kulia aliokuwa amekaa mheshimiwa mbunge na DAS wetu aliyefariki,”alisema Mganga.

Amesema mara baada ya ajali hiyo DAS alipoteza maisha hapo hapo huku wao wakikimbizwa katika hospitaliti ya Chamwino kwajili ya matibabu ambapo Mbunge alilazimika kufanyiwa upasuaji wa vidole hivyo wakahamishiwa katika hospitali ya Mkoa Dodoma (General Hospital).

Mganga amesema baada ya kupata matibabu wawili waliruhusiwa kutoka hospitalini hapo saa kumi na moja alfajiri huku mbunge Kigoda akibaki kuendelea na matibabu ya vidole alivyoumia.

Amesema katika gari hiyo ya mbunge Kigoda walikuwa watu wanne akiwemo yeye Dereva wa Mbunge Peter Mganga, Mbunge Omary Kigoda, Mbelwa Saidy ambaye ni ndugu yao pamoja na Boniface Maiga (DAS) aliyepoteza maisha na kueleza kuwa mwili wa marehemu upo katika hospitali hiyo ya Mkoa.

Credit:Majira
Watu 5 wamefariki  na 2 kujeruhiwa baada ya gari dogo aina ya Noah lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Dodoma kugongana na lori eneo la kibaigwa jijini Dodoma .

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha.

Amesema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa lori ambaye aliingia katikati ya barabara akitokea kwenye kituo cha mafuta bila kuangalia pande zote za barabara na kusababisha Noah kuingia uvunguni mwa lori. 

Pia ameeleza kuwa dereva wa lori ametoroka na jeshi la polisi linaendelea kumsaka huku likifanya uchunguzi zaidi wa ajali hiyo.

Kuhusu majeruhi wawili wa ajali hiyo Muroto amesema mmoja ana hali mbaya zaidi na juhudi za madaktari zinaendelea katika kunusuru uhai wake.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Salim Abri Asas akiwa na kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi Fortunatus Muslim wakiwajulia hali majeruhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Salim Abri Asas akiwa na kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi Fortunatus Muslim wakiwajulia hali majeruhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Salim Abri Asas akiwa na kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi Fortunatus Muslim wakiwajulia hali majeruhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MWENYEKITI wa Kamati ya Usalama Barabarani Salim Abri Asas amewashika mkono majeruhi wa ajali iliyotokea katika mlima Kitonga wilayani Kilolo mkoani Iringa na aliwaombea uponyaji wa haraka majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ruafa mkoani hapa.

Asas ameliomba Jeshi la Polisi kumtafuta na kumkamata dereva huyo aliyekimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha vifo na majeruhi kwa watanzania ambao walikuwa wamepanda basi hilo.

Alisema kitendo cha dereva huyo kutokomea kusikojulikana inaaminisha kuwa ajali hiyo ilikuwa ni ya makusudi kwakuwa angekuwepo angetoa ushirikiano mzuri kwa mamlaka zinazohusika

“Huyu dereva ni muuaji haiwezekani iwe ajali ya bahati mbaya harafu akimbie badala ya kutoa ushirikiano kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ningeomba wenzetu wa polisi wamtafute wamkamate na afikishwe katika vyombo vya sheria” amesema Salim Asas

Kwa upande wake kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi Fortunatus Muslim ametembelea majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria Kampuni ya Prezdar iliyotekea milima ya Kitonga mkoani Iringa

Kamanda Muslim alisema basi hilo lenye naomba za usajili T326 CSX Kampuni ya Prezdar linalofanya safari zake Iringa – Dar es salaam liliatumbukia katika maporomoko ya Milima ya Kitonga wilayani Kilolo.

Kamanda Muslim aliwataka madereva kutambua kuwa wamebeba roho za watu hivyo wanatakiwa kuchukua tahadhari muda wote wanapokuwa barabarani.

Alisema Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia sheria za usalama barabarani kwa kuwachukulia hatua madereva wote wanaoendelea kuvunja sharia za usalama barabarani.

Kamanda Muslim alisema jeshi hilo pia linaendelea kumtafuta na kumfikisha katika vyombo vya sheria dereva wa basi hilo ambaye alitokomea kusikojulikana mara tu ilipotokea ajali.

Watu 10 wamepoteza maisha na wengine 36 wamejeruhiwa katika ajali hiyo huku miili 5 ikiwa tayari imetambuliwa na ndugu zao


Na Editha Karlo, Kigoma
WATU tisa wamefariki  baada ya boti la abiria kuzama  katika ziwa Tanganyika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi MARTIN  OTTIENO amethibitsha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la rasini na kusema kuwa Boti ilo  liitwalo mv Nzeimana linalofanya safari zake kati ya Kijiji cha Sibwesa na ikola  limezama  likiwa abiria sitini ambapo abiria hamsini na moja wameokolewa.

Aidha Kamanda OTTIENO amesema chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali uliosababisha boti hilo kukosa muelekeo na hatimaye kupinduka.
Watu 9 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria la kampuni Kidinilo kuacha njia jana  Alhamisi Januari 9, 2020 na kupinduka eneo la Mangae barabara ya Morogoro Iringa huku chanzo kikitajwa ni uzembe na mwendokasi.

Basi lililokuwa kilitokea Ifakara kwenda Dar es Salaam lilikuwa na abiria 68  kwamba majeruhi watatu hali zao sio nzuri kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata na wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, ameeleza chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa Basi la Kidinilo kutaka kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari, Dereva huyo anaitwa Shabani Sultan (54) amekamatwa wakati akijaribu kutoroka kwa kutumia Bodaboda. 

“Kati ya majeruhi tisa walionusurika kwenye ajali ya basi la Kidinilo, wawili wamevunjika miguu, mmoja hali yake si nzuri, wengine wamepata majeraha ya kawaida wanapatiwa matibabu" - RPC, Morogoro, Wilbroad Mutafungwa.