-Awaasa kutumia fursa Za maonesho hayo kufungua masoko, uwekezani na teknolojia;

-Tanzania kutangaza bidhaa za kilimo, madini, uvuvi na utalii nchini China;

DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb), amelitaka kundi la Tanzania litakaloshiriki Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (9th China International Import Expo – CIIE) kutumia jukwaa hilo kutafuta fursa za masoko, kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kuvutia uwekezaji wenye tija kwa uchumi wa Taifa.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga washiriki hao iliyofanyika katika Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es Salaam, Mhe. Londo amesema ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo ni fursa muhimu ya kuitangaza nchi kimataifa, kuonesha maendeleo yaliyofikiwa katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika biashara ya kimataifa.

Amesema Maonesho ya 9 ya CIIE yanayotarajiwa kufanyika Novemba 5 hadi 10, 2026, jijini Shanghai, China, yatatoa fursa kwa Tanzania kushiriki katika maonesho ya nchi, biashara na kampuni, pamoja na vikao vya kuunganisha wafanyabiashara, majukwaa ya uwekezaji na shughuli za kubadilishana uzoefu. Kupitia jukwaa hilo,.

Tanzania inalenga kutangaza mazingira wezeshi ya uwekezaji yanayojengwa na amani, utulivu na nafasi yake ya kimkakati kama kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na kuongeza kuwa

itatumia maonesho hayo kutangaza bidhaa zake zikiwemo kahawa, chai, korosho na viungo, pamoja na fursa zilizopo katika sekta za madini, uvuvi na utalii,

Aidha Mhe Londo alisema kuwa soko la China lenye zaidi ya watumiaji bilioni 1.4 lina fursa kwa bidhaa bora zinazozalishwa nchini, hivyo ni muhimu kwa washiriki kutumia muda huo kuanzisha mawasiliano na wanunuzi na wawekezaji wa kimataifa.

Akitoa maelekezo kwa wajumbe wa kundi hilo kushiriki kikamilifu katika mikutano ya kibiashara kati ya kampuni na kampuni (B2B), kujenga mahusiano na wanunuzi na wawekezaji, pamoja na kuhakikisha wanawasilisha bidhaa za Tanzania kwa weledi, ubora na uadilifu na amewahimiza kutumia maonesho hayo kujifunza teknolojia za kisasa za uchakataji, viwango vya vifungashio na usimamizi wa mnyororo wa ugavi ili kuongeza thamani ya malighafi zinazozalishwa nchini.

Mhe. Londo ameishukuru Serikali ya China kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kwa ushirikiano na msaada uliotolewa katika maandalizi na usajili wa kundi hilo ma kusema kuwa ushirikiano huo unaonesha namna uhusiano wa kihistoria na kimkakati kati ya Tanzania na China unavyoendelea kuimarisha biashara, uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara, huku akiwataka wajumbe wa delegesheni hiyo kurejea na matokeo yatakayochochea mikataba ya kibiashara, ushirikiano mpya wa uwekezaji na fursa za ajira kwa Watanzania.
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: