Na Mwandishi Wetu.
Wamiliki na viongozi wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kuboresha mazingira ya kazi na kulinda maslahi ya Waandishi wa Habari, kwa kuwa usalama wa ajira, malipo ya haki na upatikanaji wa stahiki vina mchango mkubwa katika ubora na uaminifu wa habari zinazowafikia wananchi.
Wamiliki na viongozi wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kuboresha mazingira ya kazi na kulinda maslahi ya Waandishi wa Habari, kwa kuwa usalama wa ajira, malipo ya haki na upatikanaji wa stahiki vina mchango mkubwa katika ubora na uaminifu wa habari zinazowafikia wananchi.
Wito huo umetolewa leo tarehe 20 Novemba, 2026 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Wakili Patrick Kipangula, wakatu akifungua Mkutano Mkuu wa tatu wa Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.
Amesema maendeleo ya sekta ya habari hayawezi kupimwa kwa wingi wa vyombo vya habari pekee, bali kwa namna wafanyakazi wake wanavyothamjniwa, kulindwa na kuwezeshwa kutekeleza majukumu yao.
Aidha, Wakili Kipangula ameihimiza JOWUTA kuwa daraja la majadiliano na utatuzi wa changamoto, kwa kusimamia maslahi ya wanachama kupitia sheria na mazungumzo yenye tija na kwamba JAB ipo tayari kushirikiana na JOWUTA ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo endelevu, kuhamasisha uzingatiaji wa maadili ya taaluma na kujenga uelewa kuhusu haki na wajibu wa Waandishi wa Habari, kwa kuzingatia mipaka ya kisheria ya kila taasisi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa JOWUTA, Bw. Musa Juma Siwayombe, amesema chama hicho kinalenga kuhakikisha wafanyakazi wa vyombo vya habari wanapata mazingira rafiki na salama ya kazi, mikataba halali ya ajira pamoja na stahiki zao kwa mujibu wa sheria.
Ameiomba Serikali kuendelea kuimarisha mazingira ya usalama kwa Waandishi wa Habari wanapotekeleza majukumu yao, huku vyombo vya dola vikitambua nafasi yao kama washirika muhimu katika maendeleo ya Taifa.
Mkutano huo umefanyika chini ya kaulimbiu isemayo, “Mshikamano, Haki na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari.”











Post A Comment: