Mtwara: Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limewawezesha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Lindi na Mtwara kutembelea miundombinu ya gesi asilia Mnazi Bay na Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia Madimba mkoani Mtwara kwa lengo la kuwaongezea uelewa kuhusu sekta ya mafuta na gesi.

Kupitia ziara hiyo, wanafunzi wamejifunza namna gesi asilia inavyozalishwa, kuchakatwa na kusafirishwa, huku wakihamasishwa kusoma kwa bidii ili kushiriki na kunufaika na fursa zinazotokana na rasilimali za Taifa.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa TPDC, Bw. Oscar Mwakasege, amesema:

“Elimu hii inawapa wanafunzi fursa ya kuona kwa vitendo kile wanachokisoma darasani, kuelewa shughuli za sekta ya gesi asilia na kutambua nafasi yao katika maendeleo ya Taifa.”

Ameongeza kuwa TPDC inaendelea kuwekeza katika kuwafikia wanafunzi kupitia programu mbalimbali ikiwemo kuanzisha kuendeleza na kuimarisha Klabu za mafuta na gesi asilia shuleni.

Ernesta Goddess, mwanafunzi wa Kidato cha Tano kutoka Shule ya Sekondari Mtwara Girls, ameishukuru TPDC kwa fursa hiyo, akisema:

“Ziara hii imenisaidia kupata uelewa wa vitendo kuhusu shughuli za gesi asilia na kuongeza hamasa yangu ya kujifunza.”
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: